28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU yazitaka taasisi kuwasilisha taarifa fedha za miradi

Na Sheila Katikula, Mwanza

MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mwanza, Frank Mkilanya, amewataka wakuu wa taasisi mkoani hapa kuhakikisha wanawasilisha taarifa zao za mapokezi ya fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo mapema iwezekanavyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Novemba 3,2021, Mkilanya amesema ni vema kuwasilisha taarifa hizo mapema ili kuongeza uwazi kwani kila mwananchi.

“Mkibaini kuna utekelezaji mbovu wa miradi ni vema mtoe taarifa TAKUKURU, kwani kila mtu anajukumu la  kulinda fedha hizi ili miradi ikamilike mapema, kwa maana vitendo vya rushwa katika miradi  vinarudisha maendeleo nyuma,” amesema.

Amesema TAKUKURU kupitia mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu ilitembelea  miradi 74, kati  ya hiyo miradi minne  ilikataliwa na kiongozi wa mbio za mwenge.

“Miradi iliyokataliwa ni mradi wa maji  wa kata ya Ng’haya  wa Wilaya ya Magu, mradi wa mzani wa mazao ya samaki mwaloni uliopo Wilaya ya Ilemela, mradi wa bodaboda stendi ya mabasi Nansio Ukerewe  na mradi wa  maji Tabaluka Nyampande uliopo  wilayani Sengerema.

Amesema changamoto zilizofanya  miradi hiyo kukataliwa ni gharama za ujenzi kuwa kubwa ukilinganisha na uhalisia, kutokuwepo kwa nyaraka muhimu kama barua ya mapokezi ya fedha  na maelekezo  ya matumizi ya fedha na vifaa duni vya ujenzi.

“Kutokana na sababu hizo TAKUKURU imefungua majalada ya uchunguzi na tupo katika hatua mbalimbali, pindi itakapobainika kuna ubadhirifu wa fedha unafanyika wahusika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria,”amesema Makilya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles