DURBAN, Afrika Kusini
IDADI ya wanaume wanaojiua nchini Afrika Kusini ni mara mbili ya ile ya wanawake, kwa mujibu wa utafiti wa mwaka jana wa Momentum Life uliotangazwa wiki hii.
Utafiti huo umebaini kuwa kati ya watu 20 wanaoripotiwa kujitoa uhai, 17 (85%) ni wanaume, jambo ambalo Mkuu wa Kitengo cha Bima ya Maisha cha Momentum Life, George Kolbe, amesema linatia hofu.
“Licha ya kuwa na mwaka wenye changamoto nyingi (ikiwamo Corona), visa vya kujiua havijaongezeka…” amesema Kolbe na kuongeza kuwa inatia moyo kuona kiwango cha matukio ya kujiua katika taifa hilo kimeshuka kwa asilimia 39.
“Tunatakiwa tuanze kuchunguza sababu ya wanaume kukimbilia kujiua. Kama tutaanza kuona dalili na kutoa msaada wanaohitaji, basi huenda tukabadilisha hali iliyopo.”