24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyembaka mlemavu ajisalimisha polisi

PRETORIA, Afrika Kusini

MWANAUME mkazi wa Kaskazini Magharibi mwa Afrika Kusini amejisalimisha kituo cha polisi baada ya tukio la kumbaka mwanamke mwenye ulemavu wa miguu aliyekutana naye barabarani.

Wiki iliyopita, Otsile Juell Boinamo mwenye umri wa miaka 31, alikutana na mwanamke huyo (30) akiwa kwenye kiti cha magurudumu na ndipo alipomdanganya kuwa angemsaidia kumpelekea nyumbani.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi wa Kaskazini Magharibi, Adele Myburgh, Boinamo hakutekeleza ahadi hiyo na badala yake alimpeleka mafichoni na kumuingilia kwa nguvu mlemavu huyo.

Akisimulia zaidi, amesema: “Boinamo alijisalimisha mwenyewe kwa polisi Jumatatu (wiki hii), ambapo alikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya ubakaji. Alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Itsoseng Jumatano. Atapanda tena kizimbani Novemba 4 (mwaka huu) kwa ajili ya ombi la dhamana.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles