28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wanaume 100,000 wafanyiwa tohara Geita

Derick Milton, Geita

Mkoa wa Geita umefanikiwa kuwafanyia tohara wanaume 115,000 sawa na asilimia 95, kati ya wanaume 119,000ambao walilengwa kufanyiwa katika kipindi cha Oktoba mwaka jana hadi Septemba mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Japhet Simeo, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Kagera na Geita kuhusu kuandika habari za tohara yaliyoandaliwa na Shirika la IntraHealth.

Dk. Simeo amesema kufanya tohara kwa wanaume na watoto wadogo, ni moja ya kampeni inayoendeshwa na serikali mkoani humo kwa kushirikiana na IntraHealth lengo likiwa kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

“Takwimu za maambukizi ya Ukimwi zimekuwa zikipanda kutoka asilimia 4.5 mwaka 2016/17 hadi kufikia asilimia tano mwaka huu.

“Bado mkoa watu wanaoishi navirusi vya ukimwi wanaendelea kutoweka na hawajulikani walipo kutokana na wengi wao kuhama hama kutokana na shughuli za uchimbaji madini, uvuvi na kilimo.

“Mpango wetu mpya kwa sasa ni kufanya tohara kwa watoto wadogo, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa tohara kwa wanaume, lakini pia tunaviomba vyombo vya habari, kutusaidia kutoa elimu kwa wananchi kufanya tohara hasa wanaume, ” amesema Dk. Simeo.

Kwa upande wake Mshauri wa huduma za tohara kutoka IntraHealth mkoa, Dk. Peter Sewa, amesema mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara yuko kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kuliko mtu aliyepata tohara ambaye uwezo wa kutopata maambukizi ni asilimia 60.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles