30.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

THRDC waitaka serikali kurekebisha kanuni hizi za sheria

Asha Bani, Dar es Salaam

Mtandao  wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC) kwa kushirikiana na Asasi nyingine za kiraia nchini wameitaka serikali kurekebisha baadhi ya kanuni za sheria ya mashirika yasiyo ya serikali iliyofanyiwa marekebisho mwaka huu.

Akizungumzana waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 10, jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema katika marekebisho hayo kuna vipengele ambavyo vitazibana taasisi zisizo za Serikali (NGO’s) na kuzifanya kushindwa kufanya kazi zake kwa asilimia 100.

Amezitaja baadhi ya kanuni zilizofanyiwa marekebisho ambazo alieleza kuwa ni changamoto kwao ni pamoja na utoaji wa taarifa za fedha na ripoti ambayo yanaweza kudhoofisha uwezo wa mashirika yasiyo ya serikali kufadhili shughuli zao.

“Mahitaji makubwa ya kutoa taarifa za kifedha na utoaji wa ripoti ambayo yanaweza kudhoofisha mashirika kufadhili pia kuingilia shughuli za ndani za mashirika vitendo vya kuingilia haki za mashirika kufanya kazi kwa uhuru.

“Kanuni hizo zitakuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za faragha ya mashirika vitendo vinavyoingilia haki ya mashirika kufanya kazi kwa uhuru,” amesema Olengurumwa.

Naye mwakilishikutoka Taasisi ya Kutetea Demokrasia na Utawala bora yenye kituo chake Mwanza, Jimmy Luhende, amesema ni vyema Serikali ikawasikiliza na kuona umuhimu wamarekebisho ya baadhi ya vifungu vya sheria na kanuni hizo kwa kuwa zinawafunga midomo hata kuikosoa pale itakapokuwa imekosea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles