27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wanaomiliki ardhi kinyemela Muleba watajwa

Na Renatha Kipaka, Muleba

Kamati ya Uchunguzi wa Migogoro ya Ardhi imewasilisha taarifa ya uchunguzi wa mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Ilemela, Kata ya Gwanseli, Wilaya ya Muleba kwa kuwataja wanaomiliki ardhi kihalali na wasiomiliki ardhi kihalali, hivyo kutakiwa kuyarudisha maeneo waliyojimilikisha kwa Serikali ya Kijiji.

Hayo yameele\wa Juni 21, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila katika mkutano wa hadhara ambapo amewaeleza wananchi wa kijiji hicho kuwa hakuna ardhi ya kijiji itamilikiwa na mtu bila kufuata utaratibu ikiwemo kuitishwa kwa mkutano wa hadhara ili wananchi kuridhia.

Amesema kama kuna mtu atamiliki ardhi kinyume na utaratibu huo hatua zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kunyanganywa eneo hilo.

Amesema kuwa Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya Mwaka 1999, maamuzi ya ardhi ya Kijiji ambayo inatakiwa kutumika kwa ajili ya shughuli fulani au kumilikiwa na mtu ni lazima Mkutano wa Kijiji ukae ufanye maamuzi na wanakijiji wasaini na kuwa na muhtasari kwa ajili ya rejea.

Nguvila amesisitiza kutengenezwa kwa mpango maalumu wa matumizi bora ya ardhi na kusisitiza ushiriki wa wananchi wote katika mpango huo ili waweze kufahamu ni mipango ipi imepangwa kwa ajili ya matumizi ardhi ya kijiji.

Ripoti ya Kamati ya Uchunguzi iliyosomwa na Mchunguzi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Muleba, Inspekta Joseph Dishon imeeleza kuwa vyanzo vya migogoro ya ardhi katika kijiji cha Ilemela vimetokana na kutofuatwa kwa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, hivyo ili kuondoa changamoto hizo kamati ilipendekeza kuwa.

“Serikali ya Kijiji itambue Maeneo yake na kuyawekea ulinzi ili kuepusha kuvamiwa na wananchi wenye uchu wa ardhi bila kufuata utaratibu na serikali ya kijiji imeombwa kuunda kamati maalum ya kubainisha ardhi zilizorudishwa pamoja na ardhi ambazo umiliki wake haukuwa halali ili ziweze kuwekwa vizuri kwenye kumbukumbu ya ardhi ya kijiji pamoja na kuweka mipaka ya kudumu.

“Pia kwa waliojimilikisha ardhi kinyume na utaratibu warudishe ardhi hizo kwenye Serikali ya Kijiji na ardhi zitakazorudishwa zitambuliwe na serikali ya kijiji ili ziweze kuwekwa kwenye orodha ya ardhi wazi za kijiji,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles