24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mgahawa wa Halmashauri ya Kwimba wawapeleka rumande watumishi watatu

*Na Clara Matimo, Mwanza

Kasoro zilizobainika kwenye ujenzi wa jengo la Mgahawa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, zimemfanya Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Robert Gabriel, kuamuru watumishi watatu kupelekwa rumande ili kujibu ubadhilifu wa fedha katika mradi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, (wa pili kutoka mbele) akikagua jengo la mgahawa lililojengwa Wilaya ya Kwimba mkoani humo, lililogharimu Sh milioni 113 huku likiwa halijakamilika linatarajia kugharimu sh milioni 160 hadi kukamilika


Jengo la mgahawa huo ambalo lilianza kujengwa mwaka 2013 linatarajia kutumia Sh milioni 160 mpaka kukamilika ambapo hadi sasa limeishagharimu kiasi cha Sh milioni 113 huku likiwa bado linahitaji gharama kubwa ikilinganishwa zilizoikwishatumika.

Mhandisi Gabriel alifikia hatua hiyo mapema leo Juni 22, 2022 baada ya Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa MwanzaWaziri Shabani, kutoa taarifa kwenye mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani uliolenga kujadili utekelezaji wa hoja za CAG kueleza Sh milioni 137 haionekani kwenye ujenzi wa jengo hilo hali iliyomrazimu Mhandisi Gabriel kwenda kulikagua.  

Kufuatia hatua hiyo, Mhandisi Gabriel amemuamuru Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo, Mayombo Mtaju, kuwaweka rumande watumishi watatu ili watoe maelezo jinsi fedha hizo zilivyotumika huku akitaka mweka hazina naye ajumuishwe kutoa maelezo ni kiasi gani cha fedha alichoidhinisha katika ujenzi wa jengo hilo.

Waliowekwa rumande ni  Mtakwimu, Mubaraka Salumu, Mkuu wa Idara ya Mipango, Rogalevene John na Mtumishi mwenziye katika idara hiyo, Fortunata Mpuya, ambao walishindwa kujibu swali la  Mhandisi Gabriel aliyetaka kujua gharama halisi ambazo hadi sasa zimekwishatumika katika ujenzi wa mradi huo na kutoa majibu yaliyozua mkanganyiko.

Pamoja na hatua hizo alizochukua mkuu huyo wa mkoa pia ameamuru iundwe timu maalumu ya kuchunguza ubadhilifu huo huku naye akisema ataunda ya kwake ya kujitegemea ili kufanya upelelezi na utafiti wa kina wa fedha hizo.

“Uchunguzi ufanyike kwa kina, mkuu wa wilaya na mkurugenzi tafuteni nyaraka zote za jengo hili  tuwafahamu waliojenga na gharama zilizotumika, hapa nimeona hapaeleweki ukiishaona mahali hakuna lugha ya pamoja kuna mgogoro hakuna anayejua ni kiasi gani cha fedha kimeishatumika hadi sasa kulipa fundi na vifaa vya ujenzi.

“Mkuu wa idara ya mipango miji amesema hadi sasa zimetumika sh milioni 60 kumlipa fundi, mwenzie amesema Sh milioni 88, mtakwimu anasema Sh milioni 113 majibu yote hayajitoshelezi, kama mmeishatumia fedha hizo kumlipa tu fundi je vifaa vimegharimu Sh ngapi? Kuanzia kesho upelelezi wa kina ufanyike na ukamilike haraka Kwimba ni kichaka cha wizi serikali hatuwezi kuwafumbia macho watumishi wabadhilifu,” amesema na kuongeza kuwa:

“Mkurugenzi wasikuweke mbele hapa pamechafuka kusanya taarifa zote, fedha zilizolipwa nani aliidhinisha hizo fedha ili pia tuwabaini waliohusika kuidhinisha fedha hizo kabla utaratibu mwingine haujaanza kufanyika hapa hatutarudi nyuma,” amesema Mhandisi Gabriel.

Aidha, ameeleza kwamba yeye mwenyewe kitaaluma ni mhandisi amesimamia majengo makubwa ya mabilioni ya fedha hivyo akiona jengo anajua kiasi kilichotumika na hujenga mabweni yenye urefu wa kutosha kwa gharama ya Sh milioni 80 iweje mgahawa huo ambao ni mdogo ugharimu kiasi kikubwa cha fedha bila kukamilika.

Pamoja na mambo mengine mkuu huyo wa mkoa ameonyesha wasiwasi juu ya vifaa vya ujenzi vilivyotumika katika jengo hilo ikiwemo  matofali  ambapo aliamuru aondoke nayo machache ili akayapime ubora.

“By professional mimi ni engineer nikiona tu kifaa cha ujenzi najua haya matofali ninamashaka nayo tutaenda nayo machache tukayapime lakini pia nitaleta technical team kukagua, atakuja mhandisi QOS na mimi tutafuatana tutakuja kufukua msingi tupime material yote yaliyotumika kwenye ujenzi wa jengo hili tutaangalia huko chini tuone nondo zilizotumika tutaangalia kila kitu na kumbukumbu zote ziwepo kwenye eneo hili,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles