30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaofanya uvuvi haramu wakamatwa Muleba

Na Nyemo Malecela,Kagera

Kikosi kazi kilichoundwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera kimeendelea na doria za mara kwa mara na kufanikiwa kukamata watu wanaojihusisha na uvuvi haramu wakiwa na zana haramu zinazotumika kuvua samaki kiharamu, kokoro na timba zenye thamani ya Sh milioni 16 na samaki waliovuliwa kwa kutumia zana haramu hizo tani sita zenye thamani ya Sh milioni 10.

Akizungumza mara baada ya zana hizo haramu kufikishwa makao makuu ya wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Muleba ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Usalama ya Wilaya, Toba Nguvila ameendelea kuwasihi wavuvi haramu kuacha mara moja biashara hii kwani itawapelekea kubaya.

“Mtandao wa wavuvi hawa ni mkubwa na uvuvi haramu unadhoofisha sana uvuvi endelevu kwenye Wilaya ya Muleba na Mkoa mzima wa Kagera. Waliokamatwa ni mabingwa wa kuingiza zana haramu kupitia mipaka mbalimbali kutoka nchi za nje ili kuwawezesha wavuvi haramu waliopo ndani ya nchi,” amesema Nguvila.

Nguvila amesema; “Mtandao ni mkubwa sana, unahitaji umakini sana kuufutilia, unahitaji nguvu kubwa sana kwa ajili ya kuwabaini wote ili kukomesha uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria na ndani ya ziwa Burigi,” amesema.

Aidha, ametoa rai kwa wavuvi wanaojishughulisha na biashara hii haramu kuwa ni vema wakajiunga na uvuvi endelevu, uvuvi wa kihalali kwa kutumia nyavu zilizothibitishwa na Wizara na ambazo hazileti madhara katika mazalia ya samaki.

Nguvila alisema iko hatari katika uvuvi haramu itakayopelekea kupoteza mazao ya samaki kwenye maziwa, kupoteza ajira kwa waliojiajiri kupitia uvuvi endelevu na kupoteza mapato mengi ambayo Serikali inayapata kupitia uvuvi endelevu.

Pia aliwaonya wavuvi kuacha kabisa kuvua samaki walio chini ya viwango kwani kikosi kazi kipo kazini na kinaendelea na zoezi la kuwabaini na kuwakamata wote wanaojihusisha na uvuvi haramu.

“Hivyo kwa wanaondelea watakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya kisheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua kali zinazowastahili ikiwemo kufirisiwa mali zao kwani sheria ya uvuvi ipo wazi,” amesema.

Aidha, aliwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za siri na taarifa wanazotoa zitaendelea kuwa za siri ili kukabiliana kutokomeza uvuvi haramu katika visiwa 39 vilivyopo wilaya ya Muleba ndani ya ziwa Victoria na ziwa Burigi.

Pia Nguvila eleza kuwa wapo maafisa uvuvi wanaoshirikiana na wavuvi haramu kuvua samaki kiharamu na kuwasafirisha au kuwauza kiharamu hivyo aalwaonya Maafisa Uvuvi hao wasio waadirifu na waaminifu wanaoshirikiana na wavuvi haramu kuendeleza uvuvi huu kuwa watachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwani uchunguzi unaendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles