26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Timu nane zajitosa Ligi ya Wilaya Muleba

Na Nyemo Malecela,Kagera

Timu nane wilayani Muleba mkoani Kagera zimejitosa kushiriki Ligi ya Soka Wilaya inayotimua vumbi katika uwanja wa Zimbihile wilayani humo.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo jana, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila amewataka vijana kutumia mashindano hayo kujitafutia fursa za ajira kwani yatatumika kukisaka kikosi cha wilaya hiyo kitakachoshiriki ligi nyingine.

“Hatuwezi kuishia kwenye ligi ya wilaya na Mkoa, tunahitaji kushiriki ligi nyingine nje ya Kagera, inawezekana kwani siyo miujiza ni Mipango,” alisema Nguvila.

Pia Nguvila aliwaomba wadhamini wa mashindano hayo ambao ni Kasibante Media na kampuni ya Betika kudhamini michezo mingine ikiwemo netibali na riadha.

“Tunajua Kasibante Media mbali na kuibua vipaji vya vijana kupitia soka lakini pia mmefanikiwa kuibua vipaji vya walimbwende kupitia mashindano ya Miss Kagera, hivyo tunaomba udhamini huo uendelee hadi kwenye michezo mingine,” amesema.

Aidha Nguvila alikielekeza chama cha soka wilaya Muleba kisiyatumie mashindano hayo kuangalia mshindi pekee bali kiwatengeneze wachezaji bora watakaounda timu ya wilaya.

“Malengo ni kupati timu itakayoshiriki ligi daraja la kwanza na hatimaye ligi kuu na hii itawezekana kwani baada ya kumaliza ligi hii itafuata ligi ya Mkuu wa Wilaya itakayoitwa Samia Cup ambayo itahusisha michezo ya soka, netibali, voliball, mpira wa kikapu na riadha.

Vijana mnatikiwa kutambua kuwa michezo ni afya, ajira, umoja na ushirikiano hivyo mjitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo,” alisema Nguvila.

Katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo, timu ya Dear Mama Fc, iliishushia kichapo cha bao 3-0 timu Magata Fc.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles