26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yataka taji la 28, Manara atupa dongo Simba

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Uongozi wa Yanga umesema unataka kuchukua taji ya 28 msimu huu, huku Haji Manara akitupa dongo Simba kutokana na kinachoendelea.

Yanga inataraji kushuka dimbani Jumamosi Oktoba 30, 2021 kucheza na Azam katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 26,2021, jijini Dar es Salaam, msemaji wa timu hiyo, Haji Manara amesema wanataka kushinda mechi hiyo kwa sababu lengo la msimu huu ni kuchukua taji la 28 la Ligi Kuu.

Manara amesema mchezo huo utakuwa wa kiume kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili, kusheheni wachezaji wenye viwango.

“Tuna malengo yetu msimu huu, tunataka kuchukua taji la 28 la Ligi Kuu Bara, tunaiheshimu Azam kutokana na ubora wake, tumeona walivyocheza na Pyramid,” amesema Manara.

Amesema mchezo huo wameufanya kuwa maalum kwa mashabiki wao kwa kuwapelekea burudani ya muziki kutoka kwa wasanii wa bongo fleva.
Katika hatua nyingine, Manara ametupa dogo kwa Simba kuwa kila siku wakifungwa wanalalamika kusalitiwa.

Yanga itaivaa Azam ikiwa imeshinda mechi tatu mfululizo na kujikusanyia alama tisa zilizowaweka nafasi ya pili ya ligi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles