26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wazidi kulilia Bunge ‘live’

bunge3 MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM

MAHITAJI ya wananchi kutaka matangazo ya Bunge la Muungano kuonyeshwa moja kwa moja katika vituo vya televisheni na redio yamezidi kushika kasi, imebainika.

Utafiti uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) umeonyesha asilimia 92 ya wananchi wanaona kuna umuhimu wa matangazo hayo ya Bunge kurushwa moja kwa moja huku asilimia 79 wakipinga  uamuzi wa Serikali kuyafuta matangazo hayo.

Akizindua ripoti kuhusu kusimamishwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, Mkurugenzi wa MCT, Pili Mtambalike, alisema hatua hiyo inakandamiza uhuru wa habari na haki ya kupata taarifa.

Katika ripoti hiyo ambayo pia imenukuu utafiti uliowahi kufanywa na Taasisi ya Twaweza ya  Dar es Salaam, Mtambalike alisema   utafiti huo uligundua kuwa wananchi wengi walioulizwa walilalamika na kusema kuwa baada ya kufungiwa matangazo hayo hawajui kitu gani kinaendelea ndani ya Bunge.

Alisema katika utafiti huo, watu wanane kati ya 10 hawajakubaliana na kufungwa  matangazo hayo huku tisa kati ya 10 wanaona kuna umuhimu matangazo hayo yakarudishwa.

“Ripoti hii inapendekeza matangazo hayo yarudishwe  yaweze kuwasaidia wananchi wa kawaida kufuatilia mijadala mbalimbali ya bunge.

“Waandishi wa habari za bunge pia wajengewe uwezo  waweze kuandika habari hizo kwa weledi mkubwa.

“Ripoti hii inapendekeza pia kuwa kanuni za Bunge zitumike katika kukomesha tabia zisizotakiwa bungeni badala ya kuvilaumu vyombo vya habari   vinapokuwa vikitoa habari na kuonyesha kinachoendelea bungeni,”alisema Mtambalike.

Ripoti hiyo imetoa mapendekezo kwa uongozi wa Bunge hilo kutaja hadharani gharama halisi za kurusha matangazo hayo ya moja kwa moja ili wananchi waelewe.

“Tunapendekeza kuwapo mfuko maalum utakaojulikana kama Fedha za Matangazo ya Bunge (BBF) unaojitegemea, ambao utapata fedha kutoka nje na ndani ya Bunge,” alisema Mtambalike.

Ripoti hiyo pia imesema  kuwa si kweli kwamba utaratibu wa kurusha matangazo hayo haufanywi na Nchi za Jumuiya ya Madola kama ilivyoelezwa na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakati akielezea sababu za kufunga matangazo hayo.

“Katika utafiti huu tumegundua kuna nchi sita duniani ambazo zinaruhusu urushwaji wa moja kwa moja wa redio na runinga kama Australia, Uingereza, Canada, New Zeland na Samoa ambako redio ya taifa inalazimishwa na sheria kutangaza kila siku au kwa wiki, jinsi Bunge linavyofanya kazi yake zake,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles