Na Shomari Binda, Musoma
Wananchi mkoani Mara wameshauriwa kuzingatia afya ya kinywa na meno kama yalivyo magonjwa mengine yanavofatiliwa.
Ushauri huo umetolewa na Daktari wa kinywa na meno wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, Kamal Ndalahwa, ikiwa ni maadhimisho wiki ya afya ya kinywa na meno.
Amesema katika wiki itakayofikia kilele Machi 29, ambapo hospitali hiyo imejipanga zaidi katika utoaji elimu.
Dk. Kamal amesema elimu zaidi inatolewa katika kuhimiza kufanya uchunguzi na kusafisha kinywa na meno mara kwa mara ili kuepuka magonjwa.
Amesema pasipo kufanya uchunguzi na usafi wa kinywa na meno ni rahisi kupata magonjwa na kupelekea kong’olewa kwa meno.
Dk. Kamal amesema licha ya wiki hii kutumika kutolewa elimu lakini pia wanatoa huduma ya kuziba na kung’oa meno yenye matatizo.
“Kupita Mganga Mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara tumejipanga kutoa elimu ya kinywa na meno katika maeneo tofauti hapa mkoani. Tunawashauri wananchi kuzingatia uchunguzi wa afya ya kinywa na meno wakati wote kwenye maeneo mbalimbali,”amesema Dk. Kamal.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria kupata elimu kwenye kitengo cha kinywa na meno hospitalini hapo wameshukuru kupata elimu hiyo.