Na Amina Omari, Tanga
Wananchi wameshauriwa kuendelea kufuatilia kanuni za afya kama unawaji wa mikono licha ya ugonjwa wa corona kutoweka, ili kuendelea kudhibiti magonjwa mengine ambayo yanaambukizwa kutokana na kupuuzia kanuni za usafi.
Ushauri huo umetolewa na Daktari, Dickson Morrey wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya wananchi kupuuzia kanuni za kiafya.
Amesema kwa sasa kumeonekana kuanza kwa uwepo wa magonjwa ya kuhara na minyoo na hii inachangiwa Sana watu kupuuza kanuni za afya Kama ilivyokuwa kipindi cha Corona.
“Niwaase wananchi kuendelea kufuata ushauri uliokuwa ukitolewa na wataalamu wa afya kipindi cha CORONA kwani kutokana na kupuuza huko sasa tumeanza kupata case chache za magonywa ya kuhara” alisema Dk. Morrey.
Aidha, Dk Morrey amewakumbusha watumishi wa afya na maafisa Mazingira waendelee na utaratibu wa kutoa elimu ya afya ili kuendelea kuwaokoa watu wasiendelea kupata maradhi zaidi.