25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Mwanza wasaka maji usiku

img_2455-1024x683
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge

Na BENJAMIN MASESE,

UPATIKANAJI wa maji Mwanza umekuwa adimu kwa baadhi ya maeneo ikiwa ni siku chache baada ya agizo la Waziri  wa  Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge, kwa bodi mpya ya  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mwanza (MWAUWASA).

Waziri aliitaka bodi hiyo  kuhakikisha inapanua mtandao wa kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na kupunguza upotevu wa maji unaofikia asilimia 37.

Baadhi ya wakazi wa maeneo ya   Mwanza wamekuwa katika adha kubwa ya kupata huduma hiyo kwa vile   maji yamekuwa yakitoka   usiku na kusababisha wanawake kuamuka alfajiri kuyasaka kwenye vituo vya Mwauwasa na binafsi.

Baadhi ya maeneo yaliyo na adha ya maji ni Kiseke PPF, Igoma, Kishili, Nyakato Sokoni, Buhongwa, Bugarika na mengineyo huku  baadhi ya wananchi wamekuwa wakiomba mvua kunyesha ili kukinga maji.

Mkurugenzi wa Mwauwasa,  Antony Sanga  alikiri  kuwapo  tatizo hilo kutokana na  hitilafu katika baadhi ya mitambo.

Sanga ambaye hakutaka kufafanua akisema alikuwa   kikaoni, alisema ni kweli kuna hali ya upatikanaji wa maji usio wa kawaida.

Alisema mamlaka inaendelea na jitihada za kumaiza tatizo hilo na kuahidi kutoa taarifa baadaye.

Hivi karibuni Waziti Lwenga alizindua bodi mpya ya Mwauwasa na kuitaka kupanua mtandao wa huduma ya majisafi na majitaka kwa wananchi  na kupunuza upotevu wa maji unaofikia asilimia 37.

Pia aliziondolea halmashauri mbili za Ukerewe na Sengerema mamlaka ya kusimamia na kukusanya mapato ya  miradi mikubwa ya maji.

Badala yake alisema Mwauwasa ndiyo itakayohusika moja kwa moja akisema uzoefu na historia za halamshauri nyingi  nchini unaonyesha kutokuwa na usimamizi mzuri unaosababisha miradi kutokuwa endelevu.

Lwenge alisema Mwauwasa  ina jukumu la kuongeza kasi ya utoaji huduma ya majisafi kutoka asilimia 90 ya sasa na kufikia 95 ifikapo mwaka 2025.

Aliiagiza Mwauwasa kwamba ifikapo mwaka 2020 inapaswa kuwa imepiga hatua ya kusambaza miundombinu ya majitaka kutoka asilimia 25 ya sasa na kufikia 30.

JAMIN MASESE

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles