24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwakyembe aeleza umuhimu wa takwimu

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe

Na PENDO FUNDISHA, MBEYA

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema nchi inahitaji takwimu sahihi za idadi ya watu ili iweze kupanga maendeleo.

Dk. Mwakyembe aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na watendaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Mkoa wa Mbeya.

Alisema kwamba, katika kupanga maendeleo, Serikali inahitaji takwimu sahihi na hiyo itapatikana kutoka Rita kupitia kipengele cha vizazi na vifo.

“Kupitia sensa ya mwaka 2012, Tanzania imeweza kusajili watoto waliozaliwa kwa asilimia 12.5 na hiyo imeifanya kuwa miongoni mwa nchi tano za mwisho barani Afrika.

“Ukiangalia nchi imekuwa katika nafasi nzuri sana katika zoezi la utoaji wa chanjo za watoto walio chini ya miaka mitano, lakini katika usajili tunakuwa wa mwisho, hili haliwezekani.

“Mafanikio ya mahali husika yanatokana na mikakati na mipango mizuri, lakini kubwa zaidi ni idadi ya watu ambao wanatarajia kunufaika na malengo hayo.

“Kwa hiyo, kama takwimu hazitakuwapo, basi ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kwa sababu hakutakuwa na mafanikio yoyote,” alisema Dk. Mwakyembe.

Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe, wakati umefika kwa watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea  ili asilimia 70 ilizojiwekea nchi katika usajili zitimie.

“Katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa, tumepokea msaada kutoka UNICEF na kila halmashauri nchini, itapatiwa shilingi milioni 10 ili fedha hizo zitumike kutoa elimu kwa wananchi wafahamu umuhimu wa kusajili watoto,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles