24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi Afrika na Amerika ya Kusini wahudhuria ibada ya mazishi ya Castro

castro
Fidel Castro

 

HAVANA, CUBA

VIONGOZI kadhaa wa Afrika na Amerika ya Kusini jana walihudhuria ibada ya mazishi na mkutano mkubwa wa hadhara kumkumbuka aliyekuwa Kiongozi wa Cuba, Fidel Castro, aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 90.

Hata hivyo, Rais wa Marekani, Barack Obama na viongozi kadhaa wa Ulaya hawakuhudhuria ibada hiyo.

Marekani ilikuwa haijatangaza atakayeongoza ujumbe wake, huku Canada ambayo Waziri Mkuu wake Justin Trudeau alishutumiwa kwa kumtaja Castro kama kiongozi wa kipekee, ikiwakilishwa na Gavana David Johnston.

Kansela wa zamani wa Ujerumani, Gerhard Schroeder alimwakilisha Kansela Angela Merkel katika ibada hiyo.

Waziri Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras ni kiongozi pekee wa Ulaya aliyethibitisha kuhudhuria.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Teodoro Obiang Nguema wa Guinea ya Ikweta, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Uhuru Kenyatta wa Kenya walihudhuria ibada hiyo.

Aidha viongozi wa nchi za Amerika ya Kusini wakiwamo Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro na Evo Morales wa Bolivia walihudhuria ibada hiyo.

Kwa wengi katika nchi za Amerika ya Kusini na Afrika, Castro ni ishara ya shujaa aliyepinga ubeberu, kwa kumng’oa madarakani kiongozi dikteta aliyekuwa anaungwa mkono na Marekani, Fulgencio Batista.

Hata hivyo, wengine wanamshutumu kuwa dikteta ambaye sera zake za ujamaa ziliuharibu uchumi wa Cuba.

Korea Kaskazini iliyosema kuwa imempoteza mshirika wake mkubwa dhidi ya Marekani, imetangaza siku tatu za maombolezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles