33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Musoma vijijini waishukuru Serikali fedha za barabara

Na Shomari Binda, Musoma

Wananchi wa Musoma vijijini wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara jimboni humo.

Kutolewa kwa fedha hizo kumeiwezesha Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilaya ya Musoma vijijini kuendelea kutekeleza miradi yake vizuri na kwa ufanisi.

Katika bajeti ya maendelea kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021-2022, serikali imetoa zaidi ya Sh milioni 600 katika miradi ya barabara jimboni humo.

Moja ya miradi inayotekelezwa katika fedha hizo ni barabara kutoka Musoma Mjini Makojo hadi Busekera ambayo kwa sasa inaendelea kwa kilometa 5.

Licha ya fedha hizo kutoka Serikali Kuu pia fedha za mfuko wa jimbo zaidi ya milioni 500 zimeelekezwa kwenye miradi ya barabara na inasimamiwa vizuri kupitia Tarura.

Wananchi hao wakizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea miradi hiyo wamesema inatekelezwa vizuri na kwa kasi kubwa nakwamba wanaishukuru serikali.

Wamesema barabara kupitika kwa muda wote ni fursa nzuri kwao kiuchumi katika usafirishaji wa bidhaa kupeleka sokoni.

“Tunaishukuru sana serikali chini ya Rais Samia tunaona kwenye jimbo letu la Msoma Vijijini miradi ya barabara inakwenda vizuri chini ya usimamizi wa Tarura kupitia fedha inazozitoa.

“Pia fedha za mfuko wa jimbo zimekuwa na usimamizi mzuri hususan kwenye miradi ya barabara, hivyo tunamshukuru sana mbunge wetu Profesa Sospeter Muhongo,”amesema Majura Mjinja ambaye ni mmoja wa wananchi hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles