26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Sekta binafsi yatakiwa kushiriki mapambano dhidi ya UKIMWI

*TACAIDS yaingia makubaliano na TPSF

*Yasema juhudi zinahitajika kutunisha mfuko UKIMWI

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

SEKTA Binafdi nchini imetakiwa kushiriki kikamilifu katika kutunisha mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI(ATF) ili kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa ya kumaliza UKIMWI ifikapo 2030.

Takwimu zinaonyesha kuwa katika fedha za mapambano ya UKIMWI asilimia 94 inatolewa na wafadhili huku fadha ya ndani ikiwa ni asilimia 6 pekee.

Wito huo umetolewa Jumanne Februari 22, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF).

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko, akizungumza na wadau wa sekta binafsi wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF), hafla hiyo imefanyika Dar es Salaam Februari 22, 2022.

Dk. Maboko amesema bila wadau wa ndani kujitoa kikamilifu katika kushiriki kwenye mapambano hayo basi kutakuwa na changamoto katika kufikia lengo la 2030.

“Ni kweli kwamba tunaendelea kutegemea wafadhili kwa kiasi cha asilimia 94, huku sisi tukichangia asilimia 6 pekee, hivyo lazima tufahamu kwamba ipo siku hawa wanaotushika mkono wataacha kutusaidia.

“Hivyo, ni jukumu letu kuangalia ni kwanamna gani tunashirikiana na sekta binafsi katika kutuwezesha kujitegemea kwenye mapambano haya dhidi ya UKIMWI,” amesema Dk. Maboko.

Akizungumzia makubaliano ya TACAIDS na TPSF, Dk. Maboko amefafanua kuwa yanalenga kushirikiana katika kuhimiza sekta binafsi kuchangia katika mapambano dhidi ya UKIMWI.

“Kama tunavyofahamu kwamba TPSF ndiye muajiri mkubwa wa sekta binafsi kwa amana ya waajiri wote, hivyo makubaliano haya ni kuona ni kwa namna gani tunaweza kushirikiana katika kudhibiti maambukizi ya VVU na UKIMWI katika maeneo ya kazi pia kuhimiza uchangiaji wa fedha kwa vyanzo vya ndani ili kutunisha mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI(ATF).

“Lakini kusaidia kutoa elimu, kwa wafayakazi wao, umma, jamii inayowazunguka na kusaidia kufadhiri miradi mbalimbali ili kuona ni kwa namna gani sekta binafsi inakuwa na mchango kwenye mapambano haya,” amesema Dk. Maboko.

Mkurugenzi wa huduma kwa wanachama na Uwezeshaji(TPSF), Zachy Mbenna akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF), hafla hiyo imefanyika Dar es Salaam Februari 22, 2022.

Ameongeza kuwa pamoja na kwamba wafadhiri wanasaidia fedha za mapambano ya VVU lakini wamekuwa wakipunguza asilimia 5 kila mwaka.

Ameishukuru Kampuni ya Mgodi wa dhahabu ya Geita Gold Mining (GGML) kwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano ya VVU kwa muda Mrefu.

Amesema kuwa GGM na TACAIDS wamekuwa wakishirikiana kuhamasisha fedha za UKIMWI kupitia zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro (kili challange) ambapo fedha zilizokuwa zinapatikana zilikuwa zinatumika katika afua mbalimbali za UKIMWI nchini,ikiwa ni pamoja na kusaidia makundi mbalimbali yaliyoko mkoani Geita

“GGM wamekuwa wakishirikiana na sisi kuhakikisha kuwa tunatokomeza janga hili, hivyo naomba Taasisi nyingine ziweze kuiga mfano huu,” amesema Dk. Maboko.

Upande wake Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wanachama kutoka TPSF, Zachy Mbena, amesema wao kama Sekta binafsi watashirikiana na Serikali kupitia TACAIDS kuhakikisha Mapambano dhidi ya UKIMWI hapa nchini yanasonga mbele.

Amesema miongoni mwa mikakati ni kuhakikisha sekta binafsi inaangalia ni namna gani inaweza kuzalisha ARV nchini ili kupunguza gharama za kuagiza dawa hizi nje ya nchi .

“Kama ambavyo tuliweza kushiriki kwenye mapambano ya Uviko-19 basi hata kwenye UKIMWI inawezekana. Kwani tumeshuhudia kwa kiasi kikubwa nchi za Afrika ikiwamo Tanzania zikihimiza kutengeneza chanjo ya Uviko kwenye nchi zao basi hata ARVs inawezekana,” amesema Mbena.

Naye mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani(ILO, Getrude Sima amsema waoa kama Umoja wa Mataifa(UN) walikuwa wakisubiri ushirikiano huo kwa muda mrefu kwani ushirikishwaji wa sekta binafsi ni muhimu zaidi.

“Matarajio yetu nikuona wadau hawa wakikaa kwa pamoja ili kuona ushiriki wao wa moja kwa moja, kwani tumeona mfano wanaweza kununua vifaa vya watu kujipima wenyewe hatua ambayo itakuwa na mchango katika kufikia 90 90 90.

“Pia mnaweza kuandaa hata bonanza mkaleta vipimo watu wakaja wakajipima pale, hivyo niwapongeze sana kwa hiki ambacho mmeanzisha kwani kinafungua uwanja mpana sana katika kukabiliana na Mapambano dhidi ya UKIMWI,” amesema.

Sehemu ya Wanachama wa TPSF walioshiriki katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TACAIDS na TPSF yanayolenga ushirikiano katika kudhibiti maambukizi ya VVU, maeneo ya kazi pamoja na kuhimiza vyanzo vya ndani kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI (ATF), hafla hiyo imefanyika Dar es Salaam Februari 22, 2022.

Upande wake mwakilishi wa Shirikisho la wenye viwanda nchini(CTI), Neema Ngodo amesema kuwa kuna faida nyingi kwa sekta binafsi kushirikishwa kwenye mapambano ya UKIMWI na kwamba jambo la msingi ni kupatiwa taarifa.

“Mtu akijua kwamba badala ya kulipa kodi TRA anaweza kuchangia kwenye mfuko wa UKIMWI (ATF) hili ni jambo zuri na wengi wataliunga mkono, jambo la msingi nikupatiwa Elimu,” amesema Neema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles