24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Abiria wakwama kwa saa zaidi ya 20 mpaka wa Tunduma

*Chanzo chaelezwa kuwa ni foleni

Na Denis Sinkonde, Songwe

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amesema ili kuondoa kero ya foleni katika mpaka wa Tanzania na Zambia katika mji wa Tunduma kuna haja kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutengeneza barabara ya njia nne kutoka Mlowo mpaka Tunduma.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba akizungumza kwenye kikao hicho.

Mgumba ametoa kauli hiyo mapema leo Jumatano Februari 23, 2022 katika kikao cha ushauri mkoa wa Songwe(RCC) katika ukumbi wa mkoa huo uliopo Nselewa, baada ya barabara kuu ya kutoka Tanzania kwenda Zambia kuwa na foleni.

Foleni hiyo imesababisha adha kubwa ya magari ya mizigo yaendayo nchi za Kusini mwa Afrika pamoja na mabasi yaendayomikoani ikiwamo jijini Dar es Salaam.

Mgumba amesema foleni hiyo imetokea kufuatia mgomo wa madereva ulioanza Februari 14hadi 19, mwaka huu ambao umetatuliwa na viongozi wa pande zote mbili Tanzania na Zambia, hivyo magari yaliyokuwa yamepaki katika mikoa ya Songwe, Mbeya na Njombe kuanza kuruhusiwa kuingia mpakani hapo.

“Asilimia 65 ya mizigo inayosafirishwa na malori hayo yanatoka bandari ya Dar es Salaam  hivyo wizara ya ujenzi na uchukuzi ina haja ya kupanua barabara iwe ya njia nne kutoka Mlowo hadi Tunduma ili kuondoa foleni,” amesema Mgumba.

Mgumba amesema foleni hiyo imesababisha abiria wa mabasi na magari yaliyotoka Sumbawanga, Tunduma kwenda Mbeya hadi Dar es Salaam kukwama hivyo kuzua tafrani ya usafiri.

Malori yaliyokuwa yanayotoka Tanzania kwenda nchi za Kusini mwa Afrika yamelundikana  na kufunga njia kuanzia Kijiji cha Chimbuya hadi Tunduma mpakani mwa Zambia kuanzia jana Februari 22, hadi hii leo Februari 23, 2022.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles