20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Bukoba watakiwa kuchukua tahadhari ya Marburg

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Wananchi katika Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Marburg kwa kutumia njia za asili kuwafukuza wanyama pori ambao wanaishi jirani na makazi ya watu ili kuuondoa ungonjwa huo.

Rai hiyo imetolewa juzi na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Dk. Bandioti Gavyole wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali kujua njia sahihi za ya kujikinga na kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Gavyole amesema katika historia ya ugonjwa huo ni kwamba, wanyama aina ya sokwe, nyani, popo wanaishi kwenye mistu mikumbwa huwa na asilimia ya kusambaza kwani hula matunda ya pori ambayo binadamu anaweza kuyatumia na kupata ugonjwa huo.

Gavyole amesema ugonjwa huo unasambaa kwa kasi hivyo mtu anapoonekana kuwa na dalili ya homa, maumivu makali ya kichwa, mwili kuishiwa nguvu, maumivu makali ya misuli, macho kuwa mekundu, vidonda vya koo, vipele vya ngozi, maumivu ya tumbo, kutoka damu puani na kutapika damu anatakiwa kuwahi kituo cha afya haraka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Interfaith Partnership(TIP), Asina Shenduli akitoa maelekezo juu semina ya Ugonjwa wa Marburg.

Amesema endapo mtu yuko kwenye familia akatokea mgonjwa mwenye dalili hizo asitibiwe kwa kununua dawa na kujitibu pasipo kuwaona wahudumu wa afya kupata vipimo.

Amesema njia moja wapo ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo ni kujiepusha na kugusa majimaji ya mwili wa mtu kwenye dalili za ugonjwa huo.

“Jamii iepuke kusalimiana kwagusana mikono kukumbatiana au kubusiana pia watu wanawe mikono kwa maji tiririka kwa sabuni mara kwa mara, kula na kugusa mizoga au wanyama mfano popo, nyani, tumbili au swala wa msituni,”amesema Gavyole.

Saada Jumaa ambae alikuwa mshiriki katika semina ya viongozi wa dini amesema kuwa mfano yeye na wakazi wa Kata Kanyangereko nyani wanachezea hadi kwenye viyoo vya nyumba na wanajisaidia hapo hapo kitu ambacho ni hatari.

“Mimi ninatafakari tutasafishaje mazingira yetu na wakati tumesha ambiwa kwa hatutakiwi kuwa na ukaribu na hao wanyama na tufanyeje ili kuwaondoa kwenye mazingira na tuwe salama jamani na watoto wetu,” amesema Jumaa.

Afisa Ustawi wa Jamii katika Manispaa ya Bukoba ambae pia ni Mkuu wa kitengo cha usimamizi kitengo cha Saikolojia, Japhet Kanoni.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii katika Manispaa ya Bukoba ambae pia ni Mkuu wa kitengo cha usimamizi kitengo cha Saikolojia, Japhet Kanoni amewaeleza viongozi wa dini kuwatia moyo waumini wao kwa kuwaeleza ukweli ili watulie na hiyo itawaondolea msongo wa mawazo.

“Ndugu zangu viongozi wadini niwambie tu katika majanga watu huhitaji msaada wa kisaikolojia maana watu huhitaji kupata huduma ya akili, kimhemuko kijamii na kiroho kwa mtu au vikundi kwani Kuna watu ambao sio wavumili wanapo pata mshituko”amesema Kanoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles