24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ditopile aungana na wanaKongwa kwa Iftar, wamuombea dua Rais Samia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katika Muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile ameungana na Waumini zaidi ya 500 katika Msikiti mkubwa Kata ya Mkoka, Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma katika Iftari na Dua Maalum ya kuiombea nchi na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kabla ya Dua hiyo Mhe. Mbunge alitembelea Shule ya Msingi Mkoka Kitengo Maalum cha Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu(walemavu) na kuwapelekea sadaka, vitabu, kalamu na mahitaji ya shule mbalimbali.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile anaendelea kuwatakia Waislamu wote nchini Ramadhani njema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles