27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Bandari kavu ya Kwala kuanza kazi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Uchukuzi, Atupele Mwakibete ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi  wa Bandari nchini(TPA) kuhakikisha inaanza kutoa huduma kwa kutumia Bandari kavu kwa kuanza na Bandari ya Kwala ili kupunguza Shehena ya Mizigo inayosababisha msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mwakibete ameyasema hayo Aprili 1, 2023 baada ya kutembelea na kukagua  Bandari kavu ya Kwala ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 95, ambapo ujenzi wa Barabara ya zege kutoka Vigwaza mpaka Kwala yenye urefu wa kilometa kumi na tano na Ujenzi wa Reli inayoingia katika Bandari hiyo vimeshakamilika.

“Mpaka sasa Serikali  ya awamu ya sita inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan imewekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 80 kwenye ujenzi wa Bandari hii ya Kwala na miundombinu yake, hivyo naelekeza TPA anzeni kutoa huduma kupitia bandari hii mara moja ili kupunguza Mizigo na Maroli katika Bandari ya Dar es Salaam ili muweze kuvutia watumiaji zaidi wa Bandari ya Dar es salaam na kuongeza mapato,” amesisitiza Mwakibete.

Pia amekitaka kitengo cha Masoko cha TPA kutumia fursa hiyo ya kuanza kutumika kwa Bandari kavu ya Kwala kuitangaza Bandari  ya Dar es Salaam pamoja na Bandari zilizochini ya mamlaka ya Bandari nchini Kitaifa na Kimataifa ili ziweze kupata wateja wengi zaidi, kwani Bandari hasa Bandari ya Dar es Salaam inamchango Mkubwa sana katika kukuza pato la Taifa.

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mahusiano Dk. George Fasha  amesema kuwa mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kinaendelea kutangaza huduma za Bandari katika nnchi jirani kama vile Burundi, Rwanda, DRC -Kongo na zambia

Kwa upande wake Meneja Msimamizi wa Ujenzi wa Bandari ya Kwala, Alexander Ndibalema amesema ujenzi wa Miundobinu Muhimu katika Bandari hiyo umeshakamilika  kinachosubiliwa sasa ni makubalinao na mamlaka ya mapato nchini (TRA) kuhamia katika eneo hilo ili Bandari ianze kutoa huduma.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini imeshatenga maeneo kwenye mji wa Kwala mahali ilipo Bandari Kavu kwa ajili ya Taasisi Mbalimbali wezeshi  ili kuanza kutoa huduma katika Bandari ya hiyo itakapoanza kufanya kazi  na tayari watumishi ishirini wa Mamlaka ya Usimamizi  wa Bandari nchini wameshahamia Kwala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles