30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Buhigwe wafurahia kusogezewa chanjo ya Uviko-19

Na Editha Karlo, Buhigwe

WANANCHI wilayani Buhigwe mkoani Kigoma wamefurahia kusogezwa kwa huduma ya chanjo uviko-19 kupitia mikusanyiko mbalimbali jambo ambalo wamesema litawapunguzia adha ya kutembelea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.

Wakiongea kwenye mkutano wa kutoa elimu ya chanjo na kuhamasisha kuchanja Jumatatu Oktoba 18, 2021 ulioratibiwa na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na timu ya Wataalam wa Afya kutoka wilayani humo katika soko la Buhigwe, baadhi ya wananchi wamefurahi zoezi hilo na kuipongeza serikali kwa uamuzi huo mzuri.

“Tumefurahi kusogezewa huduma hii ya chanjo awali umbali wa kufuata chanjo na kukosa elimu ili kuwa sababu ya wengi kushindwa kuchanja lakini sasa hivi mambo ni mazuri kama hivi mmetufuata hapa sokoni kutupa elimu na kutuchanja hapa hapa,” amesema Martha Chiguti Mfanyabiashara sokoni hapo.

Upande wake, Ibrahimu Ndameze ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Buhigwe amesema alikuwa akizubiri kwa hamu kupata elimu ya chanjo hiyo ili aweze kuchanja na kupatiwa cheti sababu yeye ni mfanyabiashara na huwa ana safiri mara kwa mara hivyo kupata cheti cha chanjo kutamuondolea usumbufu wakati wa safari zake.

“Yaani nilipoliona tu gari la afya hapa sokoni nimefunga biashara yangu kwa muda kuja kusikiliza elimu hii ya chanjo ya Uviko-19, nina washukuru na nawashauri ambao hawajapata chanjo hii wasisite, binafsi sijaona kama kuna shida yoyote tujitokeze kwa wingi kupata chanjo hii wataalamu wetu wa afya wanapopita,” amesema.

Naye Mwandishi wa Habari wa kituo cha Star Tv Mkoa wa Kigoma, Richard Katunka amesema uamuzi wa kutoa elimu ya chanjo ya Uviko-19 na kuhamasisha wananchi kuondokana na dhana potofu ya kwamba chanjo hizo si salama.

Mwandishi wa Habari wa Star TV Mkoa wa Kigoma, Richard Katunka akiwaelewaza wananchi wa Buhigwe umuhimu wa chanjo ya Uviko-19, kwenye viwanja vya soko la Buhigwe.

Katunka ameongeza kuwa chanjo ya Uviko-19 siyo lazima inatolewa kwa hiyari lakini wananchi wanatolewa shaka na waendelee kupata chanjo kwakuwa haina madhara yoyote na inasaidia kutokupata maambukizi kwa kiwango kikubwa.

“Niwaombe ndugu zangu tupate chanjo hii kwani ni salama na watafiti wamethibitisha hili pamoja na shirika la afya ulimwenguni(WHO), sasa hivi tuna vuta hewa ya Mungu bure hatulipii, ila ukiumwa corona hewa utailipia kwa kununua mtungi wa gesi kila baada ya masaa ili kunusuru uhai wako, wangapi wanaweza mudu hizo gharama?ujanja ni kuchanja ndugu zangu,”amesema Katunka.

Naye Mratibu wa chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Stephano Joseph Mabula amesema huduma hiyo sasa inatolewa katika vituo vyote vya afya lakini pia, lakini pia wanatoa huduma hiyo kwa njia ya mkoba unaotembea ambapo huwafuata wananchi katika kaya kwa kaya na maeneo ya shughuli zao ili waweze kuwafikia wananchi wanahitaji chanjo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles