24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

ALAT kushughulikia changamoto za Serikali za Mitaa

Na Renatha Kipaka, Bukoba

MWENYEKITI wa Umoja wa Mamlaka ya Viongozi wa Serikali za Mitaa ALAT Taifa (ALAT), Murshid Ngeze amesema katika uongozi wake atashughulikia mambo ambayo ni tatizo katika serikali za mitaa hasa kwenye upungufu wa watumishi hali inayofanya kushindwa kusimamia na kukamilika kwa wakati kwa miradi ya maendeleo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya vipaumbele ambvyo atakwenda kushughulikia ili kuimalisha na kuondoa matatizo yanayobainika nyakati za ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Ngeze anasema katika maeneo yanayotekelezwa miradi ya Wananchi hushindwa kukamilika kwa wakati na kuonekana kuwa na mapungufu kutokana na kuwa na upungufu wa Wahandisi na watendaji wa vijiji.

“Kuna baadhi ya Halmashauri hazina watendaji wa vijiji ambao ndiyo wangeweza kusimamia miradi inayotekelezwa ngazi ya vijiji kwani hakuna wataalam kuangalia na kutolea taarifa ya maendeleo,” amesema Ngeze.

Aidha, amesema kuna changamoto kubwa pale inapo letwa miradi na kukuta wanaopewa kusimamia miradi hiyo sio wataaramu na matokeo yake hawawezi hata kufanya manunuzi ya vifaa katika maeneo husika.

“Niseme tu mfano katika Halmashauri ya wilaya Bukoba Wahandisi waliokuwepo baada ya kuundwa kwa wakala wa barabara mijini na vijijini walienda huko, hao ndio wangeweza kutembelea miradi ya miundombinu inayotekelezwa na kubaini mapungu yanayotokea wakati wa utekelezaji,” amesema Ngeze.

Amesema hali hiyo inafanya shughuli nyingi za miundombinu katika halmashauri kutokidhi vigezo vya garama inayokuwa imetolewa na serikali.

Ngeze ameongeza kuwa mifumo ya manunuzi imekuwa tatizo ambapo husafiri kutoka Vijijini kwenda mijini ambako garama ya vifaa hutofautiana na eneo ambalo hutekelezwa mradi.

Hata hivyo, amesema serikali za mtaa inapambana kushusha garama hiyo lakini, bado mifumo hufanya kupandisha na kuwa juu na kuchelewesha kukamilisha miradi husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles