29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wanajeshi wa Ethiopia waondoka Somalia

ethiopian-armyADDIS ABABA, ETHIOPIA

WANAJESHI wa Ethiopia wanaopigana na wapiganaji wa al-shabab nchini Somalia wameondoka katika kambi kubwa ya kijeshi huko Halgan katikati mwa jimbo la Hiran.

Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji hao wa Jihad walichuka eneo hilo muda tu baada ya wanajeshi hao kuondoka.

Mamia ya watu wameanza kulitoroka eneo hilo wakihofia mashambulio ya kundi hilo.

Hii ni mara ya tatu mwezi huu ambapo wanajeshi wa Ethiopia wameondoka katika kambi muhimu nchini Somalia.

Imedaiwa kuwa huenda wanajeshi hao wamerudi kwao kwa ajili ya kukabiliana na maandamano yanayoendelea Ethiopia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles