Ciara, Russell Wilson wanatarajia mtoto wa kwanza

0
742

ciara-harris-and-russell-wilsonNEW YORK, MAREKANI

STAA wa muziki nchini Marekani, Ciara Harris na mumewe Russell Wilson, wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mtandao wa E News, ulidai kuwa mmoja wa watu wa karibu wa familia hiyo ameuambia mtandao huo kuwa Ciara ni mjamzito na anatarajia kuitwa mama hivi karibuni.

“Ciara kwa sasa ni mjamzito na hivi karibu ataanza kuitwa mama na mume wake Russell anasema anatamani kuwa na watoto wawili au watatu akiwa na Ciara,” kilisema chanzo hicho.

Huyo atakuwa ni mtoto wa kwanza kwa Russell na wa pili kwa Ciara, huku mtoto wa kwanza, Zahir Wilburn, alizaa na mpenzi wake wa zamani Future miaka miwili iliyopita.

Ciara na Russell walifanikiwa kufunga ndoa Julai mwaka huu, mjini Liverpool.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here