25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi walia umasikini unachangia mimba za utotoni

Janeth Mushi -Arusha

BAADHI ya wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Enyoito,iliyopo wilayani Arumeru mkoa wa Arusha,wamelalamikia umaskini na baadhi ya walezi na wazazi kutokuwafuatilia maendeleo yao kuwa chanzo cha mimba za utotoni.

Wanafunzi hao waliyasema hayo juzi wakizungumza katika mdahalo wa namna ya kukabiliana na changamoto za ujana, zinazopelekea wasichana kupata mimba, mdahalo uliofanyika shuleni hapo.

Mmoja ya wanafunzi, Nanyori Lairumbe,alisema wazazi na walezi wengi wamewekeza muda mwingi kwenye harakati za kutafuta kipato na kushindwa kutenga muda wa kuwafuatilia watoto wao.

 Alisema jambo hilo linasababisha wasichana wengi kushindwa kujisimamia na kujikuta wakiingia kwenye vitendo vya ngono kwa kukosa mwongozo sahihi wa wazazi au walezi

“Unakuta mzazi anaondoka alfajiri, anarudi usiku,pengine watoto wamelala hana muda wa kuzungumza nao,anachojali ameacha chakula hivyo tunajikuta tunajilea wenyewe ama na msaidizi wa kazi ndo analea  jambo hili linawaangiza wasichana kwenye ngono na kupata mimba zisizotarajiwa,”

Esther Saiguran,alidai umasiki umekuwa ukisababisha baadhi ya wasichana kujiingiza katika vitendo vya ngono wakiwa na umri mdogo ili waweze kujikimu katika mahitaji yao mbalimbali.

“Msichana anakuja shuleni, anatembea umbali mrefu,kutokana na kutokupewa nauli hivyo wengine kujikuta wakijiingiza katika vishawishi na mitego ya wanaume na kubeba ujauzito na kukatiza ndoto zao,”alisema

Mtaalamu wa Saikolojia na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Zena Daudi aliwasihi wanafunzi wa kike licha changamoto zinazowakabili, ikiwemo hali duni za maisha ya wazazi wao kujithamini na kuepuka vishawishi.

Alisema iwapo wanafunzi wa kike watajithamini na kujikubali,wataweza kuepuka vishawishi na kufikia ndoto zao na kuwa changamoto za dunia hii ni nyingi  hivyo wana jukumu la kukabiliana nazo.

“Ukiwa na malengo na kujiamini na hali yako, huwezi kushawishika wala kujiona mnyonge na hali ya maisha ya wazazi wako, msichana hakikisha unajiamini, na kuridhika na maisha yako, usikubali umasikini wako ukudhalilishe na kukatisha malengo na ndoto za maisha yako,”

Mdahalo huo uliendeshwa na watalamu wa halmashauri ya Arusha, kwa kushirikiana na Shirika la JHPEIGO kupitia Mradi wa Tupange Pamoja, unaowezesha vijana kupata huduma rafiki na elimu ya  afya ya uzaazi, kwa ufadhili wa Mfuko wa Bill&Melinda Gate la nchini Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles