23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati za lishe zatakiwa kusaidia jamii

Samwel Mwanga ,Maswa

WAJUMBE wa kamati ya lishe Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, wametakuwa kutambua wanalo jukumu kubwa la kusaidia jamii ipate uelewa wa kutosha ili iondokane na matatizo ya watoto kupata utapiamlo,udumavu na wajawazito kupata kinga wakati wa kujifungia.

Hayo yalisemwa  na Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyonge wakati akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo.

Alisema Serikali iliamua kuanzishwa kwa kamati hizo baada ya kubaini bado kuna tatizo katika masuala ya lishe katika jamii.

Alisema  ni vizuri wajumbe wa kamati hiyo kushirikiana kutoa elimu jamii kwa kuwa lishe ni eneo nyeti linalochangia ustawi wa taifa kwa kuwa na nguvu kazi imara inayotokana afya bora.

“Wajumbe wa kamati ya lishe ni lazima mshirikiane katika kutoa elimu ya lishe katika jamii kwani suala la lishe  linachangia kwa kiasi kikubwa kuchangia ustawi wa taifa letu, jamii ikiwa na afya bora watafanya kazi ,”alisema.

Alisema  kwa uzoefu wake, ameona mikoa ambayo ni kinara wa uzalishaji wa mazao ya chakula ndiyo inakuwa na watoto wengi wenye utapiamlo na hii inatokana ya jamii kutokuwa na elimu ya lishe.

Mratibu wa Lishe wa Wilaya hiyo,Abel aliitaka jamii kuachana na mazoea hasa  matumizi ya chunvi isiyo na madini joto ambayo wananchi wengi wanaikimbilia kutokana na urahisi wa bei.

Pia aliiomba jamii kuachana na dhana potofu ya kuwazuia wajawazito kutumia vidonge vya Fefo kwa madai watapata matatizo wakati wa kujifungua jambo ambalo ni upotoshaji na inasababisha mjamzito na mtoto anayetarajiwa  hatarini kupoteza maisha wakati wakujifungua au mtoto kupata ulemavu.

Wlisema wapo tayari kwa pamoja kushirikiana na wataalamu kwenda kwenye jamii kutoa elimu kwa kuwa suala la lishe linaonekana halipewi kipaumbele na wananchi wa kawaida kutokana na kutotambaua athari zinazojitokeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles