26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Magari, nyumba vyachomwa moto

Hadija Omary -Lindi

MAGARI  saba,nyumba tatu, zahanati moja na ofisi ya kata, vimechomwa moto maeneo tofauti  mkoani Lindi.

Kutokana na hali hiyo, jeshi la polisi linawashikilia watu kadhaa kwa kuhusika na tukio hilo

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,  Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema uhalifu huo umefanyika wakati wa  uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Alisema katika Wilaya ya Liwale,  uhalibifu huo umefanywa kwa mbunge mteule wa jimbo, Zuberi  Kuchauka  ambapo nyumba zake mbili  na magari matatu  yamechomwa na moto.

Alisema mgombea udiwani Kata ya Liwale Mjini ambaye  alishinda nyumba yake imechomwa moto na zahanati yake, imevunjwa vioo vyote  na kuharibiwa baadhi ya vifaa vya  maabara.

Alisema pamoja na mali nyingine ambazo wanaendelea kuzitathmini magari hayo  saba yaliyochomwa moto, yalikuwamo ya Serikali yakiwamo yaliyopelekwa kwa ajili ya uchaguzi.

Alisema watu hao ambao baadhi yao wamekamatwa pia walikusudia kuchoma moto nyumba ya askari mmoja ambaye alikuwa akishiriki zoezo la kusimamia upigaji kura,lakini walishindwa, badala yake wakaishia kuvunja vioo vyote vya nyumba hiyo.

Alisema hali aliyoikuta baada ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa, inaacha maswali  mengi kama vurugu zote hizo ni kwa sababu ya  uchaguzi tu au kuna jamnbo jingine nyuma yake?

“Kwa  sababu vurugu zile zilianza kufanyika mapema  kabla  ya matokeo kutolewa, zilianza kufanywa saa mbili usiku hadi saa nne,wakati huo matokeo yalikjuwa bado…”alisema.

Alisema katika mji wa Nachingwea kumefanyika mambo aloyoyaita yasiyo ya kiungwana wala kibinadamu.

Alisema gari la Serikali liilichomwa moto pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ahmad Makoroganya na nyumba yake kuvunjwa vioo vyote. Makoroganya alikuwa mgombea udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),  alishinda uchaguzi huo.

Alisema pia ofisi ya Serikali ya Kata ya Mpiruka pia ilichomwa moto.

Akizungumza watu waliokamatwa kutokana na vitendo hivyo wilayani Nachingwea, Zambi alisema kundi la watu lilikuwa limejificha nyumbani kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa wa Chadema likiwa na lita zaidi ya 40 za petroli, vinyago vya kuziba uso(mask), fomu namba 3 za polisi, pamoja na vitambulisho vya kupigia kura zaidi ya 60.

Kuhusu Jimbo la Mtama, Zambi alisema ofisi maendeleo ya jamii ilichomwa moto  imeanguka haifai tena kwa matumizi, huku akisema jaribio kama hilo lilifanyika Kijiji cha Nyangamara.

Kuhusu Kilwa Kusini,alisema kulikuwa na jaribio la kuchoma ofisin ya kata ambapo petroli ilikwishamwagwa  eneo hilo, lakini  hivyo wasamaria wema waliwahi na kuidhibiti.

Alisema hadi sasa haijajulikana dhamkira ya watu wanaofanya huhalifu huo ni kina  hadi, huku wakijiapiza kuwa  wataua.

Aliyataja maeneo ambayo kauli hizo zimekuwa zikisemwa, kuwa ni Nachingwea, Liwale, baadhi ya maeneo ya Mtama na Kivinje.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles