28.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wakaribishwa Chuo cha Ustawi wa Jamii

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

TAASISI ya Ustawi wa Jamii (ISW) imewakaribisha wanafunzi wanaotaka kusoma fani mbalimbali kutembelea katika banda lake ili kujua programu mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwamo mafunzo ya muda mfupi yanahusiana na changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 17 ya elimu ya juu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Naibu Mkuu wa Taasisi ya Taaluma, Profesa Sotco Komba amesema Chuo hicho kina program zaidi ya 20 kuanzia ngazi ya cheti na Shahada ya Uzamili (Masters).

Amesema mwanafunzi akifika kwenye banda lao atapatiwa msaada wa kitaalamu juu ya fani anayotaka kusoma pamoja na kudahiliwa papo hapo.

“Taasisi ya Ustawi wa Jamii tunashiriki katika maonesho haya ya Vyuo Vikuu ambayo yameandaliwa TCU, na kikubwa tunachokifanya hapa ni kuweza kuwafahamisha wanafunzi na Watanzania kwa ujumla juu ya program zetu ambazo tunazitoa.

“Mkishafika hapa mtakutana na vitu vingi vizuri, tutawaelekeza kuhusu program mbalimbali ambazo tunazitoa, ambazo ni pamoja na zinazohusiana na mambo ya Social Work, Labour Relations na mafunzo ya muda mfupi ambayo yanahusiana na changamoto mbalimbali ambazo jamii inakumbana nayo kwa sasa ikiwemo Stress (msongo wa mawazo) katika masuala ya kazi na changamoto za kifamilia,” mesema Komba.

Aidha, amewakaribisha Watanzania kwa ujumla kutembelea taasisi hiyo iliyopo eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo pia kuna Kituo cha Elimu, Ushauri na Masuala ya kisaikolojia.

“Tunaona jamii yetu inakabiliwa na changamoto ya Sonona (msongo wa mawazo) ambapo tatizo hili limekuwa likiongezeka kila siku, kwahiyo waje kituoni kwetu kupata elimu ambayo itawasaidia na kuwarudisha katika hali yao ya kawaida ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kila siku,” amesema Prof. Komba.

Maonesho ya Vyuo Vikuu yameanza Julai 18, mwaka huu, yakihusisha vyuo vikuu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambapo yamefunguliwa rasmi jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa na yatahitimishwa Julai 23, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles