24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi waaswa kusoma sayansi

kinanaNa Patricia Kimelemeta, Muleba
WANAFUNZI wametakiwa kupenda kusoma masomo ya sayansi waweze kupata fursa ya ajira wanapomaliza masomo yao, jambo ambalo linaweza kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana alikuwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakatanga wilayani Muleba wakati wa kukabidhi kompyuta zitakazotumika kwa ajili ya masomo ya sayansi.
Alisema hatua hiyo itawasaidia kuingia kwenye soko la ushindani wa ajira ndani na nje ya nchi.

Masomo hayo ni muhimu kwa sababu yataisaidia serikali kupata watalaam watakaofanya kazi mbalimbali kwenye fani hiyo, hivyo wanafunzi wanapaswa kuhamasishwa waweze kuyapenda, alisema.
“Ninawaomba msome masomo ya sayansi ambayo yatawasaidia kuingia kwenye ushindani wa soko la ajira la ndani na nje ya nchi jambo ambalo linaweza kupunguza tatizo la ajira nchini,”alisema Kinana.
Alisema mkakati wa serikali ya CCM ni kuhakikisha idadi kubwa ya wanafunzi wanasoma hayo kuwasaidia kupata maendeleo.
Alisema dunia ya sasa ni ya sayansi hivyo kila nchi zikiwamo za Afrika, hazina budi kuwahamasisha vijana wao wapende masomo hayo waweze kuingia katika dunia ya sayansi.
Kinana alisema jamii inapaswa kushirikiana na serikali kuhakikisha mpango huo unafanikiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles