27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Vikumbo vyaanza jimbo la Ukonga

Na Humphrey Shao, Dar es Salaam
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha kompyuta, Anthony Karokola, ametangaza nia yake ya kugombea ubunge Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) .
Aliwaambia waandishi wa habari ni kwa jinsi gani anavyosukumwa na maendeleo ya wana Ukonga na kutaka kuendeleza alipoishia marehemu Eugine Mwaiposa.
“Nitamuenzi mama Mwaiposa kwa kufuata nyayo zake na kufuata mazuri yote aliyoyafanya na aliyotaka kuyafanya nitayatekeleza,” alisema Karokola.
Alisema Mama Mwaiposa alitumia baadhi ya miradi yake kusaidia jamii kama kusomesha watoto yatima katika shule yake ya Tumaini iliyopo Kitunda.
Karokola alisema Mwaiposa aliwainua katika uchumi baadhi ya wanawake ndani ya jimbo lake na nje la jimbo lake kwa kufungua Saccos ndani ya jimbo la Ukonga.
Alisema yeye kama msomi atahakikisha suala la upatikanaji elimu bora katika jimbo hilo linakamilika kuweza kupata kizazi kinachoweza kujiongoza.
Alisema kupitia utalaamu wake wa kompyuta atahakikisha kila shule ya kata inapata mwalimu bora wa kompyuta na vitendea kazi vya kisasa kusaidia vijana kwenda kasi na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Msomi huyo alisema Mwaiposa alikuwa mwanasiasa aliyekomaa katika siasa na alishirikiana na wanasiasa wenzake bali kujali itikadi za vyama.
Alisema miongoni mwa watu waliomshawishi kuingia kwenye siasa ni Mwaiposa kwa kuwa siasa zake zilikua za kujenga na kuleta maendeleo na si za chuki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles