31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 900 wanusurika kifo

Munasa NyirembeNa Pendo Fundisha, Mbeya

WALIMU na wanafunzi zaidi ya 900 katika Shule ya Sekondari ya Iyunga mkoani Mbeya, wamenusurika kifo baada ya bweni moja la wavulana la Mkwawa kuteketea kwa moto.

Moto huo ambao chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme, ulitokea juzi saa tatu asubuhi wakati wanafunzi wote wakiwa darasani wakiendelea na masomo yao.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni miaka miwili kupita, baada ya bweni jingine la shule hiyo kuteketea kwa moto, hivyo ni wazi kwamba miundombinu ya shule hiyo imechoka na inahitaji matengenezo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Munasa Nyirembe, alithibitisha kutokea  kwa tukio hilo  na kusema chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokea  bweni la Mkwawa linalochukua wanafunzi 95 na kuteketeza kila kitu.

Alisema licha ya moto huo kutosababisha  kwa wanafunzi, umesababisha hasara ya mali mbalimbali za wanafunzi, zikiwamo nguo, madaftari, vitanda na magodoro .

“Hitilafu ya umeme ni mbaya licha ya kuunguza bweni la Mkwawa na bweni la Nyerere kidogo, ingeweza kuteketeza shule nzima,”alisema.

 

Kutokana na hasara hiyo, ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha unatoa huduma kwa wanafunzi walioathirika.

“Uongozi wa halmashauri uhakikishe unawahudumia wanafunzi 95 ambao vitu vyao vimeteketea kwa moto, maana hapo walipo hawana kitu chochote ili watoto waweze kuendelea na masomo,”alisema.

 

Alisema ujenzi wa jengo na ununuzi wa vitanda utafuata, baada ya Serikali kushirikisha wadau mbalimbali kukutana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles