22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Polisi yaua watatu kwa ujambazi, wakamata bunduki ya AK 47

Liberatus SabasNA ELIYA MBONEA, ARUSHA

JESHI la Polisi mkoani hapa, limedai kuwaua watuhumiwa watatu wa ujambazi na kukamata vitu kadhaa vilivyotumika kwenye matukio ya kihalifu ikiwamo bunduki aina ya AK 47 namba 1998- AFV 0822.

Mbali na AK 47, pia wamekamata sare za Jeshi la Wananchi (JWTZ), kofia tano za kuficha sura (mask), vazi la karate na pikipiki moja yenye namba bandia za MC 983 BMK.

Vingine ni bendera mbili yeusi zenye maandishi ya kiarabu zinazotumika na makundi ya kigaidi, kisanduku cha chuma na hati ya kusafiria ya Abrahaman Athuman.

Akizungumza ofisini kwake mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema kukamatwa kwa vitu hivyo kulikuja baada ya raia wema kumtilia shaka Athuman Ramadhani kuwa anajihusisha na matukio ya kihalifu.

Alisema baada ya kupokea taarifa hizo Februari 17, mwaka huu, jeshi hilo liliweka mtego katika eneo la Engosheraton –Sinoni uliofanikisha kumnasa mtuhumiwa Ramadhani.

“Tulifanikiwa kumpekua nyumbani kwake tukamkuta akiwa na milipuko aina ya explogil TMV 6, water explosive 15, giogel kubela 10, makoti makubwa mawili na kofia ya kuficha uso,” alisema na kuongeza.

“Baada ya mahojiano alituambia kuna wenzake wawili anaoshirikiana nao kwenye matukio ya uhalifu.

“Tuliandaa tena mtego saa 5 usiku polisi na mhusika walienda eneo la Fire kwenye nyumba inayodaiwa kuishi watuhumiwa wenzake,” alisema.

Alisema baada ya askari kuwasili waligonga mlango na wakati mlango ukifunguliwa mtuhumiwa ambaye ni marehemu kwa sasa alipiga kelele za ‘Takbir’ hatua iliyowafanya wenzake ndani kuanza kuwarushia risasi polisi.

Kamanda Sabas aliendelea kueleza kwamba, askari polisi walifanikiwa kuzima jaribio hilo kwa kuwajeruhi watuhumiwa hao ambao walifariki dunia wakipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha.

“Katika upekuzi ndani ya nyumba hiyo askari walifanikiwa kukuta simu ya marehemu Mary Joseph aliyefariki kwa kupigwa risasi Februari 2, mwaka huu huko Engusheraton-Sinoni.

“Pia tulikuta kifurushi cha unga wa baruti, kisu kimoja kikubwa, karatasi zenye ujumbe wa vitisho.

Kamanda Sabasi alisema ujumbe huo ulisomeka. “Nasaha kwa Kova mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza tutakufikia wewe,” na mafuta ya kusafishia bunduki,” alisema Kamanda Sabas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles