24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yagoma kupokea ushahidi wa ‘flash’

Onesmo Ole NangoleNA JANETH MUSHI, ARUSHA

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha imekataa kielelezo cha kielektroniki ‘flash’ iliyowasilishwa mahakamani hapo na aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Steven Kiruswa katika kesi ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Longido yaliyompa ushindi, Onesmo Ole Nangole (Chadema).

Mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, Jaji Sivangilwa Mwangesi, huku  Dk. Kiruswa akiongozwa na Wakili Dk. Masumbuko Lamwai, aliiomba mahakama hiyo jana ipokee ‘flash’ hiyo iliyokuwa na maneno yaliyotolewa dhidi yake katika mikutano ya kampeni ya Chadema Oktoba, mwaka jana wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Dk. Kiruswa aliiomba mahakama kupokea flash hiyo na isikilize maneno yaliyotolewa dhidi yake na kumfanya ashindwe katika uchaguzi huo ambao alipata kura19,352, huku Ole Nangole akipata kura 20,076,wakiwa wamepishana kwa kura 724.

Alidai mahakamani hapo kuwa mikutano ya  Chadema ilikuwa ikihamasisha wananchi wasimchague kwa kuwa yeye si raia wa Tanzania, bali ni mzaliwa wa Marekani kutokana na kusoma na kufanya kazi nchini humo, kitendo ambacho kilimfanya asijue mila za kabila la Masai wala matatizo ya wananchi wa Longido.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles