23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 397 washindwa kuhitimu elimu ya msingi Tanga

Na Amina Omari,Tanga

Jumla ya wanafunzi 397 sawa na asilimia 0.73 wameshindwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2020 mkoani Tanga kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro na mimba za utotoni.

Akitoa taarifa kuhusu mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2020 na uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanzamwaka 2021, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Judica Omari amesema kiwango hicho ni pungufu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo ilikuwa 558.

Alisema kuwa hali hiyo imesababishwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa miundombinu rafiki kwa ajili ya kupata elimu, umbali wa shule pamoja na wazazi kutokuwa na utayari wa uchangiaji wa chakula cha mchana kwa ajili ya vijana wao.

“Hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kushusha kwa kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 76.44% kwa mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 71.53% kwa mwaka huu,” amesema Judica.

Aidha amesema wilaya ya Kilindi ndio inayoongoza kwa kuwa na wanafunzi 11 waliokatisha masomo kutokana na ujauzito huku utoro wakiwa 103 ikifuatiwa na Handeni yenye mimba sita na utoro wanafunzi 36.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles