26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Madarasa 155 yawakosesha nafasi wanafunzi 1,800 Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu,

Jumla ya wanafunzi 25,596 sawa na asilimia 93 ya wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2020 katika mkoa wa Simiyu, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021.

Hata hivyo wanafunzi 1,837 sawa na asilimia 6.7 ya waliofaulu ambao ni 27,433 wamekosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2021 katika mkoa huo kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa 155.

Akitangaza matokeo hayo leo, Desemba 18, Katibu Tawala Mkoa huo, Miriam Mmbaga amesema wanafunzi waliopata nafasi, wavulana ni 12,116 huku wasichana wakiwa 13,480.

Katibu tawala mkoa wa Simiyu, Miriam Mmbaga akizungumza kwenye kikao cha kuchagua wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021 kilichofanyika leo mjini Bariadi.

“Wanafunzi ambao hawakupata nafasi katika awamu hii ya kwanza ya uchaguzi, wavulana ni 635 na wasichana ni 1,202 ambao wanatoka Wilaya ya Bariadi 948, Itilima 162 na Meatu 707,” amesema Katibu tawala.

Mmbaga amewataka wakurugenzi na viongozi wengine wa halmashuari ambazo zinatakiwa kujenga vyumba hivyo vya madarasa, kuhakikisha wanaendelea na ujenzi huo ili ukamilike kwa haraka, ili ifikapo Februari mosi, 2021 wanafunzi hao waweze kuanza.

Akitoa taarifa ya ukosefu wa vyumba hivyo vya madarasa, Ofisa elimu Mkoa, Erenest Hinju amesema kuwa Wilaya ya Bariadi vijiji wanahitaji vyumba 54, Bariadi mji 30, Itilima 22, Maswa 10, Meatu 39 huku Wilaya ya Busega ikiwa haina changamoto hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles