DC Kiteto aonya wakulima na wafugaji kutokuheshimu sheria

0
364

Na Mohamed Hamad, Kiteto

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Kanali Patrick Songea, ameonya jamii za wakulima na wafugaji kuacha uhasama na kuheshimu sheria zilizopo ili kujenga mahusiano mema miongoni mwao.

Akizungumza na MtanzaniaDigital leo Desemba 18, Kanali Songea amesema kutoheshimu sheria ndiyo imekuwa chanzo cha migogoro kuibuka kwenye jamii hizo na kusababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo.

Aidha, Kanali Songea amesema amebaini kuongezeka kwa migogoro hiyo kunachangia kusuasua kwa kwa maendeleo ya wananchi na uzalishaji kwa ujumla.

Amesema migogoro ya wakulima na wafugaji Kiteto inaibuka hasa wakati wa masika na kipindi cha mavuno ambapo kwa kipindi kama hiki imeshamiri.

Katika hatua hiyo ameziagiza mamlaka za utatuzi wa migogoro kutenda haki baina ya jamii hizo na kuacha tabia za kutumia migogoro hiyo kama vyanzo vya mapato yao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here