28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

“Nivumilieni nichukue maamuzi magumu, kila pesa itaheshimiwa”-Dk. Mwinyi

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DK. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wana CCM na wananchi kwa ujumla kumvumilia wakati akifanya maamuzi magumu dhidi ya  watu wanaoshiriki kufanya vitendo vya rushwa,uhujumu uchumi na ufisadi wa mali za umma.Alisema hatovumilia watendaji wanaoshiriki vitendo vya rushwa vinavyosababishia hasara serikali.

Amesema, yapo mambo yasipofanywa kwa maamuzi magumu basi huko mbele kutakuwa kugumu na yale maendeleo ambayo yamekusudiwa kufanyika hayatofikiwa.

DK, Mwinyi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchama wa Chama cha Mapinduzi kisiwani Pemba, mkutano wa shukrani kwa wana CCM baada ya uchaguzi mkuu, katika ukumbi wa shule ya Fidel Castro mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema katika maendeleo ya watu hatokuwa na muhali kwani Zanzibar kumezoeleka tabia hiyo ambapo kila anayeguswa utaambiwa ni mtoto wa fulani ama ana undugu na watu fulani huku nchini ikiendelea kufilisiwa kwa vitendo vya uhujumu wa mali za umma.Alisema amekaa madarakani kwa mwezi mmoja na nusu lakini kila anapogusa kumejaa vitendo vya ufisadi.”Nitafanya maamuzi magumu lakini sotofukua makaburi wala kutafuta mchawi , lakini baada ya maamuzi hayo kila senti ya fedha za umma itaheshimiwa.

DK. Mwinyi pia alisema, sasa wanazungumzia miradi ya maendeleo ambayo ni miradi ya fedha nyingi ikiwa ni pamoja na miradi ya ZUSP wenye dola milion 93, mradi wa maji karibu dola milion 90, na mirandi mingine itakayokuja ya muendelezo wa ZUSP wenye dola milion 110.
Hivyo alisema, asipochukua maamuzi magumu sasa, basi fedha hizo zitafujwa na kuahidi kusimamia miradi hiyo ili waweze kupata thamani katika fedha zitakazotumika.

Aidha, alieleza kuwa, wakati wa kampeni alisema kwamba amegombea nafasi hiyo kwa dhamira moja ya kuwatumikia wananchi na kwamba sasa ameshapata uongozi hivyo anayodhima kubwa kwa Mwenyezimungu na kwa wananchi ya kutekeleza aliyoyaahidi.
“Sasa leo tukiwa tunatekeleza tuliyoyaahidi alafu kuna mtu anatubomoa, kumuacha itakuwa tumejitakia sisi wenyewe,” alisema.

Alisema, anayasema hayo kwa madhumuni ya kuwatayarisha wananchi kwa watakaokuja kuyasikia katika kipindi kifupi kijacho, kwani yapo maovu yanayofanywa na yasipowekwa sawa wataendelea kuishi katika uovu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles