27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Tulia aipongeza ORXY GAS, aitaka kufika vijijini

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (CCM), Dk. Tulia Ackson ameipongeza kampuni ya gesi ya ORYX Tanzania kwa ukuaji wake wa kimkakati na mipango yao katika kuendelea kukidhi mahitaji ya watumiaji wa bidhaa hiyo.

Dk. Tulia ameyasema hayo jana Desemba 16, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bohari ya Kampuni ya gesi ya ORYX Tanzania iliyofanyika Uyole, jijini Mbeya.

Dk. Tulia Ackson wa pili kulia, akikata utepe kuashiria kuzindua Bohari ya Oryx Gas jijini Mbeya jana, Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya ORYX Tanzania, Benoit Araman

Amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya vizuri wakati huo ikiendelea kuhamasisha utunzaji wa mazingira na pia kutengeneza fursa zaidi za ajira katika mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla.

“Ninawashukuru sana Oryx Gas kwa uwekezaji mkubwa ambao mmefanya hapa mkoani Mbeya ambao utahudumia na kusaidia mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini kama Songwe, Katavi na Rukwa.

“Tunashukuru sana kwa kuchagua mbeya mjini na sisi tumefurahi kwamba mmewekeza fedha nyingi kama mlivosema wenyewe zaidi ya dola milioni mbili tunawapongeza na pia tunawashukuru kwa sababu uwekezaji huo umeanza tangu 2012 mlianza kidogo lakini sasa soko limekuwa mpaka sasa mmefika sehemu nzuri na mmetusomea tarifa nzuri,” amesema Dk. Tulia.

Aidha, ameongeza kuwa uwezo wa kuhifadhi Depoti hadi tani 110 pia kuruhusu kuzalisha tani 35 kwa saa 8,  hii ni kukidhi ukuaji wenye nguvu katika eneo ambalo soko linakua kwa kiwango cha asilimia 15 kwa mwaka.

Dk. Tulia, pia amesifu gesi ya Oryx kwa kuunda ajira katika mikoa ya nyanda za juu kusini na Mbeya kiujumla.

“Lakini pia jambo jingine ambalo ningependa kuzungumzia ni kutusaidia kwenye eneo la mazingira ni jambo zuri sana, kwa maana kwamba mazingira yetu tunapata changamoto sababu watu wengi bado tunatumia nishati inayotumia mti, mkaa, kuni lakini sasa kukua kwa depoti hii tunaimani kuwa tutaweza kupata fursa ya kutoa elimu.

“Nasisi tutaendelea kutoa elimu kwa watu ili waendelee kutumia Oryx gas ili kupunguza uharibifu wa mazingira na kwa hivo wataacha kukata miti, sehemu nyingi watatumia gesi ambayo itatusaidia katika mazingira.

“Kwahiyo ninawapongeza sana kwenye hilo ambalo mnatusaidia kutunza mazingira kwa maana ya kuhamasisha watu watumie gesi na kwa kadri gesi inavyopatikana kwa bei rahisi na kwa urahisi,” amesema Dk. Tulia.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya ORYX Tanzania, Benoit Araman, amesema bohari ya Mbeya inasambaza kwa Mawakala wakubwa wanne, maduka yanayomilikiwa na kampuni ya gesi ya Oryx mawili na mawakala wadogo 700.

Amesema makadirio kati ya kazi zisizo za moja kwa moja na za moja kwa moja kulingana na Oryx Gesi ni zinatarajiwa kuwa 800.

Araman amesema wameamua kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika gesi, kwa sababu gesi ndiyo nishati mbadala inayoweza kutumiwa kwa urahisi na watumiaji kutokana na urahisi wake katika kusafirishwa, kupatikana, bei rahisi, rafiki wa mazingira na husaidia kupambana na ukataji miti na kuchangia katika kuboresha afya ya watumiaji.

“Tumewekeza kwa kiwango kikubwa tangu 2015, mamilioni kadhaa ya, dola milioni, tukitoa ajira kwa watanzania, na bohari 8 ambazo zimetengwa kimkakati kote nchini. Bohari hii ya Mbeya uwekezaji wake ni takriban dola milioni mbili, kimkakati iko katika mkoa wa Mbeya, kusaidia usambazaji wa Gesi ya Oryx kwenye mikoa ya jirani” amesema Araman.

Upande wake, Meneja wa Bohari hiyo, Monica Ndaki amesema kiwanda hicho kinahusika na ujazaji, uhifadhi na usambazaji wa gesi ya Oryx jijini Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi, kulingana na ubora wa viwango vya kimataifa.

Meneja wa Bohari hiyo, Monica Ndaki akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Aidha, amesem kuwa kinafanya kazi kwa kuzingatia sheria zote za serikali zinazosimamiwa na mamlaka za serikali kama OSHA, MOTO, NEMC, GCLA, WMA, TRA, na TBS na inashirikiana na Jiji la Mbeya kwa kulipa ushuru unaofaa.

“Pia tuna sera ya usalama mahali pa kazi inayosimamia usalama, ubora na utunzaji wa mazingira. Tunajivunia kuwa kiwanda hakijawahi kupata mlipuko wowote wa gesi ya mitambo au majeraha katika eneo la kiwanda,” anasema Meneja wa Bohari.

“Maboresho yote ambayo Kampuni ya gesi ya Oryx imefanya yamesaidia kukuza soko letu la gesi kutoka tani 15 kwa mwezi mnamo 2012 na kufikia  tani 302 kwa mwezi mwaka huu.

“Maboresho haya ya kiwanda yanaonekana kuwa kichocheo cha maendeleo ya mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani katika uhifadhi wa mazingira na fursa za ajira. Uwekezaji ambao kampuni ya gesi ya Oryx imeingiza umeiweka kampuni katika nafasi nzuri ya kutoa huduma bora na ya uhakika kwa wateja wake kwa miaka mingi ijayo,” amesema Monica.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles