22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

DAWASA yawaondoa hofu wakazi wa Kwembe

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Wilaya ya Kibamba imewaondoa hofu wananchi wa Mbezi Malamba mawili eneo la Kwembe Mapakani kuwa ifikapo Juni 30, mwakani, kila mwananchi  atakuwa amepata  huduma ya maji safi na salama nyumbani kwake.

DAWASA  imekiri kuwa ni kweli eneo hilo linachangamoto ya kukosa maji kwa kipilndi kirefu  lakini  tayari wameshaanza  kutandika mabomba ya inchi 4, 6 na 9 kuanzia bomba kubwa liliopo  mbezi na kuelekea katika eneo hilo ili kuwaondolea wananchi matatizo yanayowakabili.

Akizungumza na MTANZANIADIGITAL jana Desemba 18, Meneja wa DAWASA Wilaya ya Kibamba Injinia Pascal Fimbuka  alisema, DAWASA inafanya kazi hatua kwa hatua hivyo hivi sasa ni zamu ya Kwembe Mpakani kupata maji.

“Serikali ya awamu ya tano inatuelekeza kuwahudumia wananchi wote bila ya kuwabagua kwa dini au chama hivyo ifikapo Juni 30, mwakani kila mwananchi wa kwembe atakuwa amepata huduma ya maji.”alisema Injinia Fimbuka.

Alisema mradi huo wa kutandika mabomba  umeanza Desemba mwaka huu na wafaidika wa mradi huo ni  baadhi ya maeneo ya Mbezi  ikiwemo Mpigi Magoe, Msakuzi, Kingazi A na B .

“DAWASA tumejipanga kuwaondolea changamoto za maji watanzania hivyo kila mtanzania anayeishi Dar es Salaam  ajue ni lazima atapata huduma ya maji “alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles