24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wamiliki ‘daladala’ Lindi watakiwa kutopandisha nauli msimu wa Nanenane

Hadija Omary – Lindi

Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri Ardhini Mkoa wa Lindi (LATRA), imewataka wamiliki wa magari ya abiria mkoani humo wanaofanya safari zao Lindi Mjini – Mnazimmoja na wengine wanaotumia njia hiyo kutopandisha nauli kwa abiria wakati wa Maonesho ya 27 ya Wakulima (Nanenane).

Maonesho hayo ambayo kwa Kanda ya Kusini yanaanza kesho Alhamisi Agosti Mosi, yanatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.

Ofisa Mfawidhi wa LATRA, Emanuel Manase Leo amesema hayo leo Jumatano Julai 31, wakati akizungumza na baadhi ya abiria na madereva katika Stendi Kuu ya Mabasi mkoani humo baada ya kubaini uwepo wa baadhi ya wasafirishaji kuanza kupandisha nauli kwa wasafiri wanaokwenda maeneo hayo.

“Wasafiriji wanatakiwa kuzingatia taratibu, sheria na kiwango cha tozo za usafirishaji kama zilivyowekwa na mamlaka, kanuni zinaelekeza abiria anayetoka Lindi Mjini kwenda Mtange anatakiwa kulipa Sh 400, anayeshuka Viwanja vya Maonyesho Ngongo anatakiwa kulipia 800 na anayeshuka Mnazimmoja Sh 1,000 na si vinginevyo,” amesema.

Aidha, amesema LATRA itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini wanaopandisha nauli kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles