24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 29, 2023

Contact us: [email protected]

Mkurugenzi Dodoma agawa viwanja vilivyotwaliwa na serikali kwa wananchi

Mwandishi wetu

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, amekabidhi hati ya viwanja kwa wananchi 144 wa Kata ya Tambukareli ambao maeneo yao yalikuwa yametwaliwa na Serikali.

Kunambi amekabidhi hati hizo kwa wananchi hao ambao wamekuwa wakihangaika kwa miaka minne na kueleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma itahakikisha kila Mwananchi anapata haki yake kama ambavyo Rais Dk John Magufuli amekua akisisitiza kuwatumikia wanyonge.

“Leo hii hapa kuna zoezi la kutoa viwanja kwa wananchi ambao ni wahanga wa maeneo yao ambao awali inadaiwa yalitwaliwa na iliyokua mamlaka ya ustawishaji Makao makuu na kuwaacha ndugu zetu hawa wakiwa hawana maeneo.

“Kwa muda mrefu kumekua na malalamiko ya wananchi na sisi kama Jiji tulifanya tathimini ya jumla na kuona ndugu zetu hawa wana haki ya kulipwa fidia maeneo yao na hivyo leo tumemaliza kero yao ya muda mrefu kwa kuwagaia viwanja bure na watakacholipia wao ni zile tozo za kawaida za kikatiba,” amesema.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Juma Mazengo, amemshukuru Kunambi alivyolivalia njuga suala lao na kuweza kumaliza kero ya wananchi wake ambao wameteseka kwa miaka minne.

“Nimshukuru Rais Magufuli kweli tumeona jinsi gani anatetea wanyonge. Hii inaonesha jinsi gani anaziishi ahadi zake alizowaahidi wananchi wakati wa kampeni, tunayo furaha sana na hakika tumeona heshima tuliyopewa na Serikali yetu,” amesema Mazengo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,259FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles