24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Diwani CCM achaguliwa kuwa Meya Ilala

BRIGHITER MASAKI – DAR ES SALAAM.

Diwani wa Vingunguti (CCM), Omary Kumbilamoto, amechaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala baada ya kumshinda mpinzani wake katika Greyson Selestin aliyepata kura 14.

Uchanguzi huo umefanyika leo Jumatano Julai 31, katika kikao cha baraza la madiwani ambapo Kumbilamoto ameshinda kwa kura 41 kati ya kura 55 zilizopigwa ambapo hakuna kura iliyoharibika.

Akizungumza na waandishi, baada ya uchaguzi huo, Kumbilamoto amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopata na kila mmoja aliyempigia kura ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuomba ushirikiano ili waweze kufanikisha majukumu ya Manisapaa hiyo.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu  kwa nafasi  hii nilioipata na kufanikisha zoezi hili la uchanguzi kufanyika na kuisha salama, nawashukuru madiwani wote mlioweza kunipigia kura za kutosha na hata msionipigia lakini mmefanikisha haki zenu za kidemokrasia.

“Kikubwa niwaombe umoja na ushirikiano katika kufanikisha majukumu ya Manispaa ya Ilala inafanya kazi na miradi yote ya mikakati ya Mh. Rais Magufuli inatekeleza kwa wakati, nitakuwa Meya wakawaida wa kutekeleza majukumu yangu kwenu ”anasema Kumbilamoto

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles