23.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

WAKIMBIA MAKAZI YAO BAADA YA KUWAPA MIMBA WANAFUNZI

 

Na Ibrahim Yassin- Mbozi

ZAIDI ya watu watano wa Kata ya Hezya wilayani Mbozi mkoani Songwe, wameyakimbia makazi yao wakikwepa mkono wa sheria baada ya kubainika kuwapa ujauzito wanafunzi watano wa kidato cha tatu.

Hali hiyo imejulikana jana baada ya mmoja wa wanafunzi, Faines Kibona, kuumwa tumbo na alipopelekwa hospitali aligundulika kuwa na ujauzito ambao umeharibika.

Kati ya wanafunzi waliopimwa ujauzito, watano kati yao walibainika kuwa na ujauzito na walipowataja waliowapatia mimba, wanaume hao walikimbilia kusikojulikana.

Baada ya tukio hilo uongozi wa kijiji ulianza taratibu za kuwapima wanafunzi wote.

Lwitiko Mgaya, mkazi wa Kijiji cha Namwangwa, alisema kuna baadhi ya watu wazima ambao wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi kwa kuwapa zawadi mbalimbali na kuwaingiza katika uhusiano wa kimapenzi na baadaye kuwapa ujauzito.

Mgaya alisema watu wote watakaobainika kuwapa mimba wanafunzi wanatakiwa wasakwe popote walipo ili wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuwa wamekatisha ndoto za wanafunzi hao.

Mama mzazi wa Fainesi, Christina Kibona, alikiri mtoto wake kuwa na ujauzito na kwamba mwanamume aliyempa mimba hiyo ametoroka.

Ofisa Elimu wa Kata ya Hezya, Juliana Mwaghamba, alisema zaidi ya watu watano wamekimbia makazi yao na wengine kukimbia na wanafunzi hao ili kupoteza ushahidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles