Na WALTER MGULUCHUMA- KATAVI
JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi, wamewaua watu wanne wanaodhaniwa kujihusisha na ujambazi wakiwa na bunduki mbili za kivita zikiwa na risasi 27.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benedictor Mapujila, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5:00 usiku katika eneo la Kahenze, Kata ya Ugala, Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, baada ya watuhumiwa hao kujibizana na polisi kwa kuwarushia risasi.
“Siku moja kabla ya kuuawa kwa majambazi hao, walimpora mtu mmoja, Shija Masanja ambaye ni mfanyabiashara simu za Tecno na fedha taslimu Sh 800,000 na kutokomea kusikojulikana.
“Katika msako huo, polisi waliwaona majambazi hao wakiwa wamejificha kichakani kando ya barabara na baada ya kugundua wanafuatwa na askari walianza kuwafyatulia risasi askari na katika majibizano hayo ya risasi yaliyodumu kwa dakika 15 polisi waliwaua majambazi wanne na kukamata silaha kadhaa ikiwamo SMG zenye namba UA 5538 1997 ikiwa na risasi 14 kwenye magazine na nyingine yenye namba AFV 0826 1996 ikiwa na risasi 13 kwenye magazine.