24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

BIDHAA FEKI ZAATHIRI VIFAA VYA UJENZI

Na ASHA BANI

-DAR ES SALAAM

IMEELEZWA kuwa soko la bidhaa za ujenzi limekumbwa na tatizo la bidhaa feki zilizo chini ya viwango na kushusha viwango vya ujenzi wa taifa pamoja na kuhatarisha usalama wa Watanzania.

Hayo yalielezwa jana na Mtendaji wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Nabaki Afrika inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya ujenzi, Princely Glorious, wakati akizindua tawi jipya linalofahamika kwa jina ‘Super Branch’ lililoko Boko jijini Dar es Salaam.

Glorious alisema kuna bidhaa zisizo halisi zinashusha viwango vya ujenzi wa Taifa pamoja na kuhatarisha maisha ya Watanzania watakaoishi au kutumia majengo yaliyojengwa chini ya viwango.

Alisema kampuni yao ya Nabaki Afrika imekuwa ikipambana na ukithiri huo kwa takribani miaka 24 na kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata bidhaa bora na halisi.

“Kampuni yetu inaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada kubwa zinazoendelea kuondoa bidhaa feki, magendo na viwango vya chini katika soko kupitia Shirika la Viwango la Taifa (TBS) na Tume ya Ushindani (FCC) tunaomba waendelee kufanya hivyo,” alisema Glorious.

Aliongeza kuwa wamekuwa wakipambana na bidhaa feki hasa kwa vigae aina ya Decra ambavyo wafanyabiashara wengi wasioitakia mema nchi wamekuwa wakiiga.

Alisema kampuni hiyo pia inauza bidhaa zake kwa kuzingatia ubora na bei kwa walaji wa aina zote.

Kampuni hiyo kwa sasa ina matawi matano ambayo ni Boko ‘Super Branch’ Mikocheni, Kariakoo, Masaki na Arusha, lakini lengo likiwa kusambaa nchi nzima.

Naye Mratibu wa programu ya kutoa mafunzo kwa mafundi kupitia Kampuni ya Nabaki Afrika, Jesse Madauda, alisema mbali na kuuza vifaa lakini pia wamekuwa wakifadhili mafundi kupata mafunzo mbalimbali na wateja wanaweza kuwapata kwa kupitia mitandao pia.

Alisema lengo la kutoa mafunzo kwa mafundi hao ni kumrahisishia mteja kupata fundi mwenye uzoefu na kazi ambaye atafanya bila kuharibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles