28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Waliovamia nyanda za malisho Kiteto wapewa siku mbili kuondoka

Na Mohamed Hamad, Kiteto

Serikali imewataka wakulima, waliovamia eneo la malisho Kijiji cha Amei wilayani Kiteto mkoani Manyara kuondoka kwa kuwa sio eneo salama.

Hatua hiyo imetokana na mtu mmoja kupoteza maisha, akidaiwa kulima eneo la malisho na kusababisha wafugaji kukosa maeneo.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Jeseph Mkirikiti akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Amei chenye mgogoro huo aliwataka wakulima waliolima eneo hilo waondoke.

“Serikali hatuwezi kulinda hawa wananchi huku… hili eneo ni hatari sana, hata haya magari kufika huku ni kazi haswa…nimetembea kutoka barabarani kuja hapa kwa zaidi ya masaa mawili usalama wenu uko wapi, hata huyu aliyeuawa hapa angepataje msaada,”alisema RC Mkirikiti.

Alisema kama kuna chakuvunwa sasa hivi wakulima hao wavune na iwe kwa siku mbili tu baada ya hapo Serikali itachukua hatua kwa watakaokaidi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, aliyefika Kijiji cha Amei wilayani Kiteto aliwataka wakulima kuheshimu maeneo ya malisho.

“Kiteto mna mpango wa matumizi bora ya ardhi, ili kuepuka migogoro kila mtu aheshimu eneo la mwenzake kuepuka mgogoro,” alisema Ndaki.

Alisema, Kiteto ilitulia miaka mitano iliyopita, lakini hivi karibuni tumeanza kusikia mauaji yanatokea kati ya wakulima na wafugaji.

Mkuu wa wilaya yabKiteto, Kanali Patrick Songea akizungumzia msimamo wa Serikali alisema Serikali inasimamia kauli moja tu, waliolima eneo la malisho waondoke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles