23.6 C
Dar es Salaam
Thursday, May 9, 2024

Contact us: [email protected]

Biden na Putin wajadili uhusiano wa Washington na Moscow

Washington, Marekani

Rais wa Marekani, Joe Biden amezunguza kwa njia ya simu na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin na kujadili masuala kadhaa ikiwemo mkataba wa kudhibiti silaha na kuwekwa kizuizini kwa Alexei Navalny. 

Kulingana na Ikulu ya Marekani, wakati wa mazungumzo hayo rais Biden, amemweleza Putin juu ya wasiwasi alionao kuhusu kukamatwa kwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Urusi, Alexei Navalny, tuhuma kuwa Moscow ilihusika na shambulizi la mtandao la hivi karibuni dhidi ya Marekani na madai kwamba Urusi imewalipa wanamgambo kuwauwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.

Kwa upande wa Ikulu ya Kremlin yenyewe taarifa yake imejikita kuzungumzia majibu ya Putin kwa pendekezo la Biden la kurefusha mkataba kati ya Marekani na Urusi wa kudhibito silaha nzito unaofahamika kama New START.

Ijapokuwa taarifa kutoka Washington na Moscow zimetilia uzito mambo tofauti, pande zote lakini zimeashiria kwamba mahusiano kati ya Urusi na Marekani walau katika siku za mwanzo za utawala wa Biden yataongozwa na shauku ya kutochochea mivutano lakini vilevile bila ya kuharakisha kumaliza tofauti zilizopo baina ya mataifa hayo hasimu tangu enzi ya vita baridi.

Kuhusu suala la mkataba wa New START marais hao wawili wamekubaliana wajumbe wa kila upande wakamilishe haraka makubaliano ya kurefusha kwa miaka mitano utekelezaji wa mkataba huo wakati muda wa sasa utakapofikia mwisho mnamo mwezi unaokuja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles