24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Foundation yaipiga tafu hospitali ya Mloganzila

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imepokea msaada wa vifaa tiba vinavyogharimu dola za Marekani 31,524 sawa na Sh milioni 73 kutoka Korea Foundation for International Healthcare (KOFIH) kwa lengo la kusaidia hospitali kuendelea kutoa huduma bora na za kibingwa.

Msaada huo ni pamoja na vifaa 14 vya kupima kiwango cha joto mwilini (Non-contact Infrared Thermometer), mashine 8 zitakazotumika kupima kiwango cha dawa kinachotakiwa kwenda kwa mgonjwa (Infusion Pump), vifaa 3 vitakavyotumika kuonesha mfumo wa upumuaji na mapigo ya moyo ya mgonjwa (Patient Monitor) vifaa 16 vya kupimia na kuwekea dawa (Nebulizer) na mashine moja ambayo inatumia kisu cha umeme kufanya upasuaji (Electrosurgical Unit).

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dk. Julieth Magandi akizungumza lo Januari 27, baada ya kupokea msaada huo, ameishukuru KOFIH kwa kuendeleza mahusiano na MNH-Mlonganzila pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuendelea kuboresha sekta ya afya nchini.

“KOFIH mmekuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada wa vifaa tiba kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma katika hospitali yetu, mwaka jana mlifanikisha mafunzo kwa wataalamu wetu kwa njia ya mtandao ya namna ya kutumia baadhi ya vifaa ikiwemo mashine ya kuvunja mawe kwenye figo na mfumo wa mkojo kwa njia ya mawimbi mshituko (Extracorporeal Shock Wave Lithotripsy ambayo ilikua ni muhimu sana na hii ni hatua kubwa,” amesema Dk. Magandi.

Pamoja na hayo, Dk. Magandi pia ametumi fursa hiyo kumshukuru Daktari Bingwa mshauri wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kutoka Korea Kusini, Prof. Huh Seong kwa mchango wake katika Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kwani amesaidia upatikanaji wa machine inayotumia kisu cha umeme kufanya upasuaji (Electrosurgical Unit).

Kwa upande wake Mwakilishi msaidizi kutoka Taasisi ya Korea Foundation for International Healthcare Tanzania, Jungyoon Kim amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana kwa karibu katika kutoa msaada na mafunzo kwa wataalamu pale itakapohitajika.

Agosti, mwaka jana KOFIH walitoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 331.3 na kuendesha mafunzo ya mwezi mmoja kwa wataalamu wa vifaa tiba kutoka mikoa mbalimbali nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles